Tuesday, November 26, 2013

USHAURI WATOLEWA KUHUSU TAASISI ZA KIFEDHA KUWAWEZESHA WATU MASIKINI


2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema pamoja na  baadhi ya viongozi wa Serikali wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere kwa ajili kufungua mkutano wa Majadiliano na Wiki ya Sera za kuondoa Umaskini, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo. 
IMG_6192
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano wa wiki ya Sera za kuondoa Umaskini, unaoendelea  kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Zainul Mzige).

Taasisi za fedha kwa kushirikiana na Serikali zimetakiwa kubuni mbinu bora za kuwawezesha wananchi wasiokopesheka ili kuwainua wananchi wa kipato chini nchini. MOblog inaripoti.
Akizungumza na wageni waalikwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa Majadiliano ya wiki ya Sera ya kuondoa Umaskini jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Mhe, Dkt. Mohammed Gharib Bilal amesema kutokana na sababu mbalmbali, watu maskini wana nafasi finyu ya kupata fursa na kuzitumia kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

“Katika suala la kukuza uchumi na kupunguza umaskini, fursa ni nyenzo muhimu zinazowezesha kufikia malengo. Fursa hizi zinaweza kuwa ni za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Hata hivyo, si watu wote wanaweza kujua fursa zilizopo,” amesema Dkt. Bilal
Amesema kuwa kukosekana kwa fursa wanazostahili kuzipata watu masikini kunaweza kuwa kumesababishwa na sababu nyingi, kama vile za kimazingira, kisera, kisheria, kiuchumi, kiutawala na kijamii.
Dkt. Bilal alilisitiza mkutano huo una historia ndefu tangu ulipoanza kufanyika mwaka 2002 lengo lao limebaki kujikita katika kutoa fursa kwa wananchi kuchambua na kujadili mafanikio, changamoto na kutafuta suluhisho lenye kulenga kuyafikia malengo.

“Nitumie fursa hii kuwakumbusha washiriki wa mkutano huu kuwa, agenda ya kuondoa umaskini si ya kitaifa pekee, bali ni ya kimataifa. Tangu mwaka 1993, Umoja wa Mataifa umetenga siku ya tarehe 17 Oktoba ya kila mwaka,” aliongeza Dkt. Bilal
Amesema katika harakati za kupambana umasikini Serikali ina programu mbalimbali kama Dira ya Taifa ya Maendeleo na Mkakati wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi (MKUKUTA) zenye lengo la kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya umasikini.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Mhe Saada Salum amesema mjadala utakuwa wa siku tatu na kauli mbiu “Kupanua wigo katika kutumia mifano bora na fursa zilizopo kwa maendeleo endelevu yenye kunufaisha watu wengi walio maskini’

Amesema kuwa mijadala mingine ni pamoja na uimarishaji wa sekta ya kilimo, masuala ya bajeti na umuhimu wake katika kutekeleza miradi na program zinazogusa maendeleo ya watu na masuala ya hifadhi za jamii.
Kwa Upande wake Afisa Maendeleo Mkuu wa Ubalozi wa Canada na Kaimu Mwenyekiti wa kikundi cha Wadau wa Maendeleo Patricia McCullagh amesema mkutano huo ni fursa ya kipekee kwa wadau wa maendeleo kuzungumzia njinsi ya kuondoa umaskini nchini Tanzania.
IMG_6135
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania  Bw. Phillipe Poinsot akifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hayupo pichani).
IMG_6174
Naibu Waziri wa Fedha Mh. Saada Salum akizungumza na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa wiki ya kuondoa umasikini jijini Dar es Salaam.
IMG_6148
Picha juu na chini ni Afisa Maendeleo Mkuu wa Ubalozi wa Canada na Kaimu Mwenyekiti wa kikundi cha Wadau wa Maendeleo Patricia McCullagh akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wiki ya Sera za kuondoa umasikini jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwamba Tanzania inajukumu la kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuzungumzia vikwazo ambavyo ni vizingiti vya Maendeleo ya Kiuchumi ya Taifa.
IMG_6153
IMG_6143
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi za Kiraia nchini Tanzania Bw. John Ulanga ambaye alizungumzia umuhimu wa ushirikishwaji wa Asasi za kiraia katika mapambano ya kuondoa umaskini.
IMG_6168
Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka mashiika ya Umoja wa Mataifa na Taasisi mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
IMG_6163
Wadau mbalimbali wa maendeleo wanaohudhuria mkutano huo.
IMG_6145
IMG_6138
IMG_6223
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal akibadlishana mawazo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Lennarth Hjelmaker, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Majadiliano na Wiki ya Sera za kuondoa Umaskini, unaoendelea jijini Dar es Salaam.
IMG_6225
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About