Sunday, December 15, 2013

HALI YA USALAMA SINGIDA YAZIDI KUA TETE, MAJAMBAZI YAVAMIA HOTELI


DSC04900
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na tukio la ujambazi mkoani Singida.
Na Nathaniel Limu, Singida
 Mfanyakazi wa Hoteli ya kitalii  ya Lake Hill Singida Motel iliyopo mjini hapa pamoja na walinzi watatu wa kampuni ya ulinzi ya binafsi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kuvamia hotel ya Lake Hill Singida Motel na kisha kupora wapangaji wawili mali mbali mbali pamoja na fedha taslimu.

Mfanyakazi wa Lake hill hotel anayeshikiliwa ni Alistided Salvatory (24) na wengine ambao ni walinzi wa kampuni binafsi ya Mass Security, ni Jumwa Mwangwi (35), Zakaria Pstory (23) na Donald Samsoni (19).
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo la uporaji limetokea Desemba tisa mwaka hu saa 9:30 usiku huko hotel ya Lake Hill Singida motel.
Alitaja wapangaji walioporwa mali zao kuwa ni Alex Fabian (59) mkazi wa Mbweni na raia wa Pakistani Rohan Yakubu (44) ambao inaelekea walikuwa wamelengwa.

“Vitu vilivyoporwa ni simu tatu za mkononi zenye thamani ya shilingi 1,020,000= saa mbili za mkononi moja yenye thamani ya dola 500 za marekani, (nyingine thamani bado haijajulikana).Pia wamepora fedha taslimu 800,000/= na dola za kimarekani 500”,alisema.
Akifafanua juu ya uporaji huo, Kamwela amesema siku ya tukio watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao idadi yao bado haijajulikana wakiwa na bunduki walivamia hoteli hiyo na kisha kufanya uporaji.

Amesema watu hao walipofika katika hotel hiyo walifyetua risasi hewani kwa lengo la kuwatisha wapangaji na walinzi waliokuwa kwenye hoteli hiyo.
“Walifanikiwa kuwafunga kamba ya katani walinzi wote watatu na hatimaye kuingia katika vyumba viwili na kufanya unyang’anyi huo”,alifafanua zaidi.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About