Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, December 2, 2013

JESHI LA POLISI LAKAMATA BUNDUKI 1 NA RISASI 13 ARUSHA

GEDSC DIGITAL CAMERA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari (Hawapo pichani) bunduki aina ya Shortgun iliyokutwa nyumbani kwa mtu anayejulikana kwa jina na Jumanne Abdallah Maarufu kwa jina la Babu G (25) Unga Ltd jijini hapa ambaye anatuhumiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya ujambazi hapa nchini. 
(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
GEDSC DIGITAL CAMERA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akionyesha risasi zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa wa ujambazi Jumanne Abdallah maarufu kwa jina la Babu G maeneo ya Unga Ltd jijini hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).

Mtu mmoja anayetuhumiwa kwa ujambazi ajulikanaye kwa jina la Jumanne Abdallah  Maarufu kwa jina la Babu G (25) Mkazi wa Unga Limited jijini hapa amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa akiwa na bunduki aina ya short gun pamoja na risasi 13 zinazotumika katika bunduki ya aina hiyo.
Bunduki hiyo yenye namba C. 056900 iliyokuwa imekatwa kitako na mtutu ilikutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, maeneo ya Unga Limited katika Halmashauri ya jiji la Arusha mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa toka kwa raia wema.

“Mara baada ya kupata taarifa, askari wetu walikwenda katika nyumba hiyo muda wa saa 2:30 asubuhi na kumkuta mtuhumiwa katika chumba chake ambaye kwa wakati huo alikuwa anajiandaa kutoka, ndipo walipomkamata kisha kufanya upekuzi katika chumba hicho na kuikuta silaha hiyo pamoja na risasi hizo”. Alisema Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas.

Kamanda Sabas aliendelea kusema kwamba, mara baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa, alikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu kama vile unyang’anyi wa kutumia nguvu na silaha katika maeneo mbali mbali hapa nchini huku  akiwataja wenzake ambao wanaendelea kutafutwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
Kufuatia mafanikio makubwa yanayopatikana ndani ya Jeshi hilo Mkoani hapa katika kudhibiti vitendo vya uhalifu, Kamanda Sabas ameendelea kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa jeshi hilo.

Pia ametoa shukrani zake kwa Maafisa, Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa jeshi hilo mkoani hapa kwa kujituma na kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa hali inayosababisha kujenga imani kwa wananchi ambao wanaendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop