Wednesday, December 4, 2013

KINANA ALITIKISA JIJI LA MBEYA


1. Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, mjini Mbeya jioni hii
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii, Des 4, 2013 katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimoisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
112
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi wa Zahanati katika kijiji cha Chamwengo Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya vijijini wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika ziara yake ya wilaya ya mbeya vijijini, Katika ziara hiyo Kinana anafuatana na wajumbe wa halmashauri kuu taifa Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa kimataifa na leo anaendelea na ziara hiyo Jimbo la Mbeya Vijijini kabla ya kumalizia kesho ambapo anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe mjini Mbeya
2
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chamwengo kata ya Inyala.
3
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala wakiwa katika ujenzi wa zahanati hiyo.
4
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala akiliweka sawa tofali wakati akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chamwengo kata ya Inyala.
5
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua tanki la maji linalojengwa katika kijiji cha Itimu kata ya Iwindi Mbeya vjijini.
6
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na mjumbe mmoja wa mabalozi wakati alipokuwa akielekea kufungua shina la CCM mjini Mbalizi.
8
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanachama waliojiunga na chama hicho wakati alipofungua moja ya matawi ya chama hicho mjini Mbalizi.
9
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wananchama waliojiunga katika tawi hilo.
11
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake pamoja na viongozi wenzake wakielekea kwenye mkutano wa ndani.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About