Monday, December 2, 2013

LG YAZINDUA VIYOYOZI VYA KUFUKUZA MBU DAR


01
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics wa Afrika Mashariki, Moses Marji (kushoto), Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala na Meneja Masoko wa LG, Soyoung Lee, wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa viyoyozi vya kufukuza mbu viitwavyo ‘LG Mosquito Away’ jijini Dar es Salaam leo.  
02
Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala akihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya uzinduzi wa viyoyozi vya kufukuza mbu viitwavyo LG Mosquito Away jijini Dar es Salaam leo.  
03
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics wa Afrika Mashariki, Moses Marji (katikati), Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alshaaf, Aliraza Rajani wakifanya mahojiano na waandishi wa habari katika uzinduzi wa LG Mosquito Away jijini Dar es Salaam leo.

Kampuni ya vifaa vya teknolojia ya LG Electronics ya Afrika Mashariki leo imezindua viyoyozi vya kufukuzia mbu iitwayo “LG Mosquito Away” na katika harakati za kupambana na vimelea vya mbu na ugonjwa wa malaria nchini 

Akizugumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics, Moses Marji amesema kiyoyozi hicho kipya kinatoa mawimbi ambayo yanaweza kumfanya mbu kuanguka na kisha kufa baada  ya muda mfupi.
“kifaa kipya ni kizuri kwa mapumziko ya nyumbani au ofisini na kinampa mteja nafasi ya kupumzika na kwa maslahi mapana ya kupambana na mbu katika maambukizi ya ugomjwa wa malaria nchini,” amesema.

Marji amesema kuwa kifaa hicho kimetengezwa mahsusi kwa mazingira ya Tanzania na Afrika mashariki kiasi ambacho kitamwezesha Mtanzania wa kawaida kumudu kununua kwa kujinga na mbu waenezao malaria.
Kwa upande wake, Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo kikuu cha Sayansi na Tiba Cha Muhimbili (MUHAS), Dakta Billy Ngasala amesema baada ya utafiti juu ya wadudu wa malaria ndipo wakashirikiana na LG kuja na mbinu mpya ya kumuangamiza mbu hapa nchini.

Amesema kwamba taasisi ya MUHAS kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa viwango vyao walifanya utafiti Bagamoyo kwa mbu ili kubadilisha mbinu ya kupambana mbu na kudhibiti ugonjwa wa malaria.
“tulifanya utafiti juu ya ugonjwa wa malaria na jinsi ya kudhibiti ugonjwa wa malaria katika harakati za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo ili kuja na mbinu mbadala badala ya dawa peke yake,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alshaaf Bargain Centre, Ali Raza kwamba bei ya kiyoyozi ni kwa mujibu wa soko la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Amesema kuwa kiyoyozi kimetengezwa kwa kumlenga Mtanzania na kwa mazingira ya nchi ni nafuu kwa matumizi na rahisi kutumia kwa watu wote.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About