Thursday, December 19, 2013

SHERIA YA KUDHIBITI UHALIFU KTK MTANDAO KUTUNGWA


cyber 01
Mkurugenzi wa TEHAMA  wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  Dkt. Ally Simba akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Patrick Makungu (hayupo pichani)  katika ufunguzi  wa kongamano la siku mbili kuhusu sheria  ya mtandao jijini Dar es Salaam.
cyber 02
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  Profesa Patrick Makungu akifafanua jambo wakati akifungua kongamano la siku mbili kuhusu sheria ya mtandao ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali wa mtandao, kongamano hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
cyber 03
Baadhi ya wadau wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la siku mbili kuhusu sheria  ya mtandao jijini Dar es Salaam.
cyber 04
Mtoa mada wa kwanza katika kongamano la siku mbili kuhusu sheria  ya mtandao Bw. Said Kalunde akitoa mada iliyohusu uhalifu wa mtandao jijini Dar es Salaam.
cyber 05
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini kongamano la siku mbili kuhusu sheria  ya mtandao jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo).

Serikali yaendelea kushirikisha wadau mbalimbali wa mitandao ili kuweza kupata sheria itakayosimamia matumizi  salama ya mitandao hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la siku mbili jijini Dar es Salaam mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu alisema kuwa serikali inashirikiana na wadau mbalimbali nchini na nje ya nchi kwa lengo la kupata maoni yao.
“Kongamano hili linakutanisha wadau muhimu ambao maoni yao yataweza kufanikisha kupatikana kwa sheria ya mtandao ambayo itakuwa ndiyo suluhisho la uhalifu wa mtandao ambao unaonekana kushamiri sana hapa nchini na duniani kwa ujumla,” alisema Profesa Makungu.

Aidha Profesa Makungu aliongeza kuwa katika kupambana na uhalifu wa mtandao Tanzania imeandaa miswada mitatu ya sheria ya usalama wa mtandao  ambayo pia inatumika katika Shirikisho la Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC).
“Sheria hizo ni sheria ya mtandao, sheria ya usalama wa taarifa na sheria ya biashara mtandao kwa kufanya hivi tuko sambamba na Jumuiya ya afrika Mashariki, Shirikisho la Maendeleo Kusini mwa Afrika na Umoja wa Afrika ambao wote wana lengo moja la kupambana na uhalifu wa mtandao,” aliongeza Profesa Makungu.

Naye Mkurugenzi wa TEHAMA toka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  Dkt. Ally Simba alisema kuwa kama hakuna  sheria ya mtandao ni rahisi uhalifu wa mtandao kupunguza wawekezaji  kwani usalama wa fedha unakuwa ni mdogo.
Serikali inaendelea  kukusanya  maoni ya wadau mbalimbali kuhusu sheria ya mtandao kwani mchakato wa kupata sheria uko katika hatua za mwisho na ambapo mwakani  katika miezi ya mwanzoni sheria hii itakuwa tayari.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About