Welcome to our online store Portal

Template Information

Friday, December 6, 2013

TANZANIAONE NA STAMICO ZAINGIA UBIA KUSHIRIKIANA


saini
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Gray Mwakalukwa (kushoto) na  Mwenyekiti wa  Kampuni ya Madini ya TanzaniaOne(kulia )  Balozi Ami Mpungwe  wakisaini hati za mkataba wa ubia  kuhusu uchimbaji  wa pamoja wa madini ya Tanzanite katika kitalu c kwenye eneo la Mererani. Sherehe hizo zilifanyika mjini Dar es salaam.
badilishanaa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Gray Mwakalukwa (kushoto) na  Mwenyekiti wa  Kampuni ya Madini ya TanzaniaOne(kulia ) Balozi Ami Mpungwe  wakibadilishana hati za mkataba wa ubia  kuhusu uchimbaji  wa pamoja wa madini ya Tanzanite katika kitalu c kwenye eneo la Mererani. Sherehe hizo zilifanyika jana mjini Dar es salaam.
KM Madini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi (kushoto)  akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo mjini Dar es salaam wakati wa halfa fupi ya kusaini hati za mkataba wa ubia  kuhusu uchimbaji  wa pamoja wa madini ya Tanzanite katika kitalu c kwenye eneo la Mererani kati ya Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na TanzaniaOne . wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Gray Mwakalukwa (katikati) na  Mwenyekiti wa  Kampuni ya Madini ya TanzaniaOne(kulia ) Balozi Ami Mpungwe.
TANZANIAONE1
Mwenyekiti wa  Kampuni ya Madini ya TanzaniaOne(kulia )Balozi Ami Mpungwe  akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo mjini Dar es salaam wakati wa halfa fupi ya kusaini hati za mkataba wa ubia  kuhusu uchimbaji  wa pamoja wa madini ya Tanzanite katika kitalu c kwenye eneo la Mererani kati ya Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na TanzaniaOne . Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)Gray Mwakalukwa.(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dar es salaam).

Shirika la Madini la Taifa [STAMICO] limeingia mkataba wa ubia na Kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited [Tanzanite One] kuhusu uchimbaji wa pamoja wa madini, ya Tanzanite katika kitalu C, Mirerani.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO Gray Mwakalukwa wakati akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari mara baada ya hafla fupi ya kusaini mkataba huo.
Mwakalukwa alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kutoa leseni ambayo inawawezesha STAMICO  kumiliki asilimia 50 na TanzaniaOne watabaki na  asilimia 50.

Alisema kuwa umiliki huo unatokana na Serikali kusimamia utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ambapo chini ya sharia hiyo, Kampuni za kigeni haziruhusiwi kumiliki hisa zaidi ya asilimia 50 katika uchimbaaji wa vito.
Mwakalukwa aliongeza kuwa mkataba huo umezingatia makubaliano ya awali yaliyotiwa saini mapema mwaka huu ambayo yataka STAMICO na Tanzanite One kuwa  na gawio sawa la asilimia 50 kwa hamsini litakalotokana na faida. 
Alitaja baadhi ya mambo waliokubaliana ni pamoja na mitambo ya uchimbaji na uzalishaji itabaki kuwa ni mali ya Tanzanite One itaendelea  kutumika na wabia wataifanyia matengenezo itakapoharibika.

Mwakalukwa alisema kuwa jambo jingine waliokubaliana ni pamoja na kuanzisha kitengo maalum cha ufuatiliaji na tathmini ya shughuli zote za mgodi kitakachoundwa kutoka kwa wajumbe wa kila pande.
Naye Mwenyekiti wa Tanzanite One, Balozi  Ami Mpungwe alisema kuwa hatua ya Kampuni yake kusaini  mkataba huo ni sehemu ya  kutekeleza sera ya uchimbaji  wa madini nchini na ni  hatua nzuri  ya  kuhakikisha ulinzi na usalama madini ya Tanzanite.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop