
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tigo Tanzania Bw. Deon Geyser
akionyeshea waandishi wa habari tuzo ya mtandao bora wa mwaka 2013
walioshinda kutoka kwa umoja wa makampuni ya simu GSMA katika kongamano
la mawasiliano na mitandao ya simu Africa Com, iliyofanyika Capetown
Afrika Kusini mwezi Novemba. Kushoto ni Mkuu wa Mipango na Uboreshaji wa
mitandao kutoka Tigo Bi. Halima Idd.

Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tigo Tanzania Bw. Deon Geyser na Mkuu wa
Mipango na Uboreshaji wa mitandao kutoka Tigo Bi. Halima Idd
wakionyeshea waandishi wa habari tuzo ya mtandao bora wa mwaka 2013
waliyoshinda kutoka kwa umoja wa makampuni ya simu GSMA katika kongamano
la mawasiliano na mitandao ya simu Africa Com, iliyofanyika Capetown
Afrika Kusini mwezi Novemba.

Mkuu
wa Mipango na Uboreshaji wa mitandao kutoka Tigo Bi. Halima Idd
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo ya
mtandao bora wa mwaka 2013 waliyoshinda kutoka kwa umoja wa makampuni ya
simu GSMA katika kongamano la mawasiliano na mitandao ya simu Africa
Com, iliyofanyika Capetown Afrika Kusini mwezi Novemba. Kulia ni Mkuu wa
Idara ya Uendeshaji kutoka Tigo Tanzania Bw. Deon Geyser.
Kampuni
ya Tigo Tanzania imeshinda tuzo ya kuwa mtandao wa simu ulioboreshwa
zaidi katika mwaka 2013 barani Afrika. Tuzo hiyo iliyotolewa katika
kongamano la umoja wa makampuni za mawasiliano duniani, GSMA,
liliyofanyika mwezi Novemba mjini Capetown, Afrika Kusini.
Akizungumzia
tuzo hiyo, Mkuu wa Idara ya Oparesheni za Mtandao na Uhandisi Tigo,
Bw. Deon Geyser, amesema kwamba kutunukiwa tuzo hiyo ni heshima kubwa si
tu kwa kampuni ya Tigo Tanzania bali pia ni udhihirisho tosha kwamba
kampuni hii inaendelea kuwekeza katika ubora; wa huduma za mawasiliano
na kutafuta suluhu katika changamoto mbali mbali zinazokumba sekta hiyo.
“Tumewekeza
kwa kiasi kikubwa ndani ya mwaka uliopita katika kuongeza ubora wa
huduma zetu za mawasiliano ili kufanya huduma zetu kupatikana kwa
urahisi na kuwa wa kutegemewa zaidi kwa wateja wetu. Tigo hivi sasa
inapatikana kila sehemu nchini na katika ubora mkubwa zaidi, kwa maana
hiyo tuzo hii ni sherehe ya mafanikio makubwa kwetu,” alisema.
Kwa
mujibu wa Bw. Geyser, maboresho hayo ya Tigo yanatokana na uongozi wa
kampuni hiyo kuamua kuja na mkakati maalum ambao ulianza kutekelezwa
wake Desemba 2012 katika idara zote husika.
“Mkakati
huu umeweza kuleta matokeo chanya kama kupunguza kukatika katika kwa
mtandao kwa asilimia 70, kupunguza kwa kukatika katika kwa simu kwa
asilimia 63 na kuongezeka kwa kasi ya kupitisha data kwa asilimia 300,”
aliongeza Geyser.
“Tigo pia imewekeza sana
katika upanuzi wa mtandao wake na kuongeza minara zaidi ili kuweza
kufikia sehemu nyingi zaidi vijijini na kuwahudumia wateja mbali mbali
katika mikoa yote 30 nchini Tanzania bara na visiwani. Kuwepo kwetu nchi
nzima inaruhusu wateja wetu kuweza kufurahia huduma zetu za kupiga simu
katika ubora mkubwa zaidi wa sauti, kuunganishwa kwa ufanisi zaidi
katika vifurushi vyetu vya data na intanet kupitia 3G, pamoja na kupata
huduma za uhakika kwenye kutuma na kupokea pesa – Tigo Pesa bila kuwa na
shida ya mtandao, masuala ambayo huwafanya wateja wetu kuwa na sababu
nyingi zaidi za kutabasamu,” alielezea Geyser.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Maboresho ya Mtandao Tigo
Bi. Halima Idd aliongeza kwamba kampuni hiyo ya simu iliweza kufanikiwa
kwa kujikita katika mkakati wao maalum wa ‘Programu ya Maboresho ya
Ubora wa Mitandao’ pamoja na kuwekeza fedha na rasilimali zingine katika
sehemu muhimu zenye kuweza kuleta matokeo yenye uhakika.
“Katika
utafiti tuliokuwa tukifanya kwa wateja wetu, mrejesho tuliokuwa
tukipata ulikuwa unahusu zaidi ubora wa mtandao wetu, tukaona ni vyema
tukalivalia njuga suala hili ili kuweza kupata suluhu ya uhakika. Hii ni
kwa sababu Tigo ni kampuni ambayo inawasikiliza wateja wake, na ni
desturi yetu kubuni bidhaa na huduma mbali mbali ambazo wateja wetu
wenyewe wamezipendekeza katika tafiti tunazozifanya mara kwa mara,”
alisema Bi. Idd.
Aliendelea, “Mkakati huu
maalum wa ‘Programu ya Maboresho ya Ubora wa Mitandao’ ulioanza mwaka
2012 ulijumuisha kuwekeza katika uwezo, upanuzi minara na ‘back up’ wa
mtandao. Pia tulibadilisha mwenendo wa utekelezaji wa miradi yetu ya
mtandao wetu na kuboresha namna ya ufanyaji kazi katika shughuli za kila
siku kwenye idara yetu ya oparesheni, uhandisi na mitandao. Lakini haya
yote yasingeweza fanikiwa kama tungesahau kuboresha mpangilio wa
ufanyaji kazi ndani ya kampuni yetu na kuwekeza katika ushirikiano,
mambo ambayo yameweza kutupa matokeo haya ambayo tunayoyafurahia sasa.”
Mwezi
Septemba mwaka huu, Tigo ilianzisha msafara ujulikanayo kama ‘Tigo
Smile Tour’ ambayo ulikuwa unapita nchi nzima ukisherehekea uwekezaji
wake katika uboreshwaji wa mtandao, pamoja na kuzindua minara zaidi ya
280 iliyowekezwa katika mikoa yote 30 nchi nzima ndani ya mwaka huu.
Uwekezaji
huu mkubwa wa Tigo pia umetoa nafasi kubwa za ajira kutokana na
kuongezeka kwa matawi mapya ya Tigo yanazotoa huduma kwa wateja katika
sehemu tofauti tofauti nchi nzima, pia kuongezeka kwa mawakala wa Tigo
Pesa, kitu ambacho ni cha muhimu sana katika kuwajumlisha Watanzania
katika maendeleo ya kiuchumi. Pamoja na haya, upatikanaji wa huduma za
Tigo pia umepanuka nchi nzima kutoka na kampuni hiyo kuongeza kwa
ufanisi mkubwa sehemu ambazo huduma zake zinaweza kupatikana kwa sasa
tofauti na zamani.
Africa
Com ni kongamano na maonyesho kubwa kuliko zote Afrika inayojumuisha
makampuni ya simu na mawasiliano kila mwaka, safari hii mkutano huu
ulifanyika Cape Town, Afrika Kusini tarehe 13 na 14 Novemba.
Tuzo za mwaka huu zilitolewa katika makundi 14 tofauti zikiwemo, Suluhu
katika Kuunganishwa Mitandao, Masoko kupitia mtandao wa simu, Muziki wa
Kidigitali na Kutuma na Kupokea fedha kupitia simu.
0 comments:
Post a Comment