Welcome to our online store Portal

Template Information

Friday, January 10, 2014

MASHINE ZA EFDs NI KUWAKANDAMIZA WAFANYA BIASHARA ASEMA WAZIRI KIGODA


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Serikali imekiri mfumo wa ulipaji kodi na ule wa utumiaji wa mashine za kutolea risiti(EFDs) kuwa ni mbovu na hivyo unahitaji kufanyiwa kazi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, amesema mfumo wa ulipaji kodi nchini bado unakabiliwa na matatizo ambayo hayawezi kusaidia katika kumuendeleza mfanyabiashara zaidi ya kumkandamiza.
Dk Kigoda alisema hayo wakati alipokutana na wafanyabiashara wa mikoa yote nchini, kuhusu maboresho katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kodi na tozo mbalimbali wanazotozwa wafanyabiashara, wajasiriamali na mapendekezo ya uendeshaji wa biashara nchini.
Alisema baada ya serikali kulitambua hilo hivi sasa inajipanga kutafuta ufumbuzi utakaosaidia kumaliza changamoto hizo. Hata hivyo, bado kuna kazi kubwa ya kupata mfumo bora wa uendeshaji biashara na ulipaji kodi.
“Suala la mashine za kutolea stakabadhi mmelizungumzia kwa mapana, lakini hata hivyo bado zina changamoto lakini haya yote mliyoyazungumza wakati nikienda kukutana na wenzangu endeleeni na kufanya biashara zenu kwa utaratibu wenu wa zamani hadi ufumbuzi utakapatikana,” alisema Dk Kigoda.
Dk Kigoda alisema kama mtakumbuka kuna taarifa zilizowahi kutolewa na vyombo vya habari kimataifa kuwa Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi iliyofanya vibaya katika kipindi cha mwaka jana kutokana mfumo mbaya uliosbabishwa na sababu mbalimbali ikiwamo masuala ya ukusanyaji kodi.
Aidha, aliwataka kuwa wavumilivu wakati matatizo yao yakishughulikiwa kwani watambue matatizo ya kiuchumi hayatatuliwi kwa migomo, maandamano ya kisiasa bali hutatuliwa kiuchumi.
“Tanzania tuna tatizo kubwa sana na lazima tuliondoe hili siyo lingine bali ni kutoaminiana kati ya serikali na wafanyabiashara. Hili lazima tulitatue kwa sababu serikali tunaona wafanyabiashara ni wajanja wanaweza kukwepa kodi wakati wafanyabiashara nao hivyo hivyo….” alisema na kuongeza:
Huku akishindwa kuweka wazi akiepuka kulizungumzia kwa undani suala la EFD, zaidi akiwapongeza wafanyabiashara hao kwa kauli yao kuwa hawapingi kulipa ko.iN Aliwasihi suala hilo litakwisha baada ya kikosi kazi kitakachoundwa kikiwashirikisha wafanyabiashara hao.
“Hatuwezi kumkamua ng’ombe atoe maziwa bila kumpa majani na hatuwezi kumaliza matatizo ya uchumi kwa maandamano au kuwasikiliza wanasiasa. Njia pekee ya kutatua matatizo haya ni kushirikisha wataalamu wa uchumi” aliongeza.
Dk Kigoda alisema waraka uliotolewa na wafanyabiashara utafanyiwa kazi na haki itatolewa baina ya mfanyabiashara mkubwa, wa kati na mfanyabiashara mdogo
Alisema serikali itaunda kikosi kazi kitakachoshirikisha jumuiya hiyo ya wafanyabiashara ili waweze kuwekeza katika mazingira mazuri.
Dk Kigoda alisema kupitia utaratibu huo ni vyema wakaangalia mfumo wa ulipaji kodi uwe ni mfumo unaoendeleza biashara na sio mfumo unaotoa kodi ili zitumike.
“Kupitia utaratibu huu ni vyema tukaangalia mfumo wa ulipaji kodi uwe ni mfumo wa kuendeleza kodi na sio kulipa kodi ili tutumie na kwamba hapa tutakaa kikao na wenzangu na wa TRA na Wizara ya Fedha na baada ya hapo tutatoa tamko”alisema Dk Kigoda na kuongeza
“Nawahakikishia mimi kama waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara lengo langu kubwa ni kusukuma serikali katika punguza gharama za biashara kwa wafanyabiashara na changamoto yetu hii ya utumiaji wa mashine hizi tutamaliza kupitia taratibu za kiuchumi”alisema
Katika hatua nyingine, Waziri Kigoda
Waziri Kigoda amewatetea wafanyabiashara wadogo manaofanya baishara zao katika maduka ya Kariakoo kwa kusema kuwa wanachangia pato la taifa katika kukuza uchumi.
“Wafanyabaishara wadogo ndio wanaochangia pato la taifa katika kukuza uchumi wa nchi tofauti na wafanyabaishara hao wakubwa na hata hivyo wafanyabaishara hao wakubwa walianzia kama hao wafanyabiashara wadogo”aliongeza.
Pia amewakalipia askari wanaofanya doria katika soko la Karikaoo maarufu kama “Tigo” kutoka na wafanyabaishara hao kudai kuwa askari hao wamekuwa tishio kwa kuwakamata bila kufauata utaratibu.
Mwakilishi kutoka Zanzibar
Mwakilishi kutoka Zanzibar Lacky Zahoor alisema tatizo kubwa ni ulipaji wa kodi katika nchi hiyo kwamba huko Zanzibar mashine hizo hwazihitaji kwa sababu zina tunza kumbukumbu zao sio hasara zao.
“Sisi tupo tayari kulipa kodi lakini mfumo uboreshwe uwe mzuri kwa ni hizi mashine kwetu Zanzibar hatuzitaki kwa sababu hazionyeshi hasara tunayopata sisi zaidi ya kumbukumbu zao tu hivyo hatuzikubali”alisema Zahoorn
Mshauri wa Jumuiya wafanyabiashara wa Kariakoo, Johnson Minja alisema chimbuko linaloonekana kuwa mzigo kwa wafanyabiashara hao ni kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuingia katika awamu ya pili ya utumiaji wa mashine hizo za kukusanyia kodi, bila kufanya tathimini ya kutosha juu mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa awamu ya kwanza ya utumiaji mashine hizo
Baadhi ya maduka katika soko la Kariakoo jana yalifungwa kutokana na wafanyabiashara hao kuhudhuria mkutano na kusababisha usumbufu kwa wateja waliofika eneo hilo la Kariako kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Hata hivyo wafanyabiashara hao walitofautiana kwani kwa upande wa wafanyabiashara wa maduka ya nguo wengi wao hawakufungua huku wa vifaa vingine kama vya ujenzi walifungua maduka.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara waliuofungua maduka walisema kuwa wenzao wengi hawajafungua kutokana na kushiriki katika mkutano.
Rehema Ahmed mmoja wa wafanyabiashara hao alisema kuwa viongozi wao waliwataka wasifunge maduka lakini kutokana na mkutano huo kuwa na umuhimu waliamua wengi wao kufunga maduka.
Mkutano huo ulihudhuriwa na zaidi ya wafanyabiashara 3500 kutoka kila kona ya nchi ikiwemo wa wakilishi kutoka Tanzania Visiwani.
Wafanyabiashara hao walianza kuwasili majira ya saa tatu na nusu asubuhi huku waziri wa Viwanda na biashara akiwaziri katika ukumbi huo saa 5:15 asubuhi.
Wafanyabaishara hao walikuwa na vipeperushi vilivyokuwa vimeandikwa “Kodi bila mashine inawezekana

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop