MKUU WA JESHI LA POLISI NA NAIBU WAKE WAAPISHWA RASMI

MKUU WA JESHI LA POLISI NA NAIBU WAKE WAAPISHWA RASMI


3
IGP mpya wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Polis wa Afrika Mashariki, Uliofanyika katika Hoteli ya Serena, Kampala,Uganda uk (1)
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna Abdulrahman Kaniki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza leo, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).
Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Share this product :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger