Welcome to our online store Portal

Template Information

Thursday, January 16, 2014

ZITTO ASEMA USHINDI WA KESI YAKE NI USHINDI WA WAPENDA SIASA SAFI NA WASIOPENDA UDHALIMU

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Baada ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kuibuka kidedea katika pingamizi lake la kuvuliwa uanachama hivi karibuni, macho na masikio sasa yameelekezwa kwenye hatima yake ndani ya chama hicho.
Akisoma hukumu hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za Wakili Albert Msando na kuipiga marufuku Kamati Kuu ya Chadema au chombo chochote, kujadili uanachama wa Zitto hadi kesi ya msingi itakapotolewa uamuzi.
“Nakubaliana na hoja za Wakili Msando, pande mbili zinapopingana lazima shauri lao lisikilizwe mahakamani ili haki itendeke.
“Mdai akivuliwa uanachama, akapoteza nafasi yake ya ubunge, Serikali italazimika kufanya uchaguzi mdogo, kufanya uchaguzi mdogo ni hasara kwa Serikali kwani utahusisha hadi wapiga kura hali itakayosababisha fedha nyingi kutumika, itakuwa hasara kwa Zitto kupoteza nafasi mbili, ya ubunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kabla kesi yake ya msingi haijasikilizwa,” alisema.

Akizungumza na mtandao wa ‘Millardayo.com’ baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, Zitto anasema ushindi huo ni kwa Watanzania wanaopenda siasa safi.
“Kwanza nataka niseme wazi kabisa kwa Watanzania ambao ni wanachama wa vyama vingine, wasio na vyama na kwa wanachadema, ushindi huu siyo ushindi dhidi ya Chadema, ni ushindi kwa Watanzania wote wanaopenda siasa safi, wanaopenda taratibu za utawala bora zifuatwe kwenye taasisi zetu, ni ushindi dhidi ya wanaotaka kukandamiza demokrasia ndani ya vyama, ni ushindi dhidi ya wahafidhina wasiotaka mabadiliko katika vyama,” anasema Zitto na kuongeza:
“Huu siyo ushindi dhidi ya chama kwa sababu siwezi kushindana na chama changu, ni chama ambacho kimenilea na nimekitumikia kwa muda wangu wote, zaidi ya nusu ya umri wangu ambao nimeishi... Kwa hiyo salamu ambazo napenda wananchi wazifahamu ni kwamba tunahitaji kuheshimu sana demokrasia na misingi ya haki za binadamu.”
Wakati viongozi wa Chadema wakimpiga marufuku Zitto kujihusisha na kazi zozote za chama wala wanachama wengine kumpa ushirikiano, mwenyewe anasisitiza yuko tayari kufanya kazi hizo.
“Mimi bado ni mwanachama wa Chadema, pamoja na kwamba Katibu Mkuu wa Chadema ametoa amri ya watu wasinipe ushirikiano lakini pale nitakapohitajika nitafanya shughuli za Chadema, nitafanya shughuli za nchi yangu,” anasema na kuongeza:
“Sasa hivi kuna masuala makubwa kuhusu Katiba ya nchi yetu na ningependa wananchi wajielekeze huko.

Akitoa ufafanuzi, Wakili na Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Peter Kibatala anasema shauri hilo lilifunguliwa likiwa na sehemu kuu mbili yaani shauri la msingi na maombi madogo ya zuio la muda.
“Katika shauri kuu, mwombaji anaiomba Mahakama Kuu kutoa amri tatu; kwamba Chadema izuiwe kujadili suala la uanachama wake mpaka pale atapopewa nakala za mwenendo na uamuzi wa Kamati Kuu kumvua nafasi za uongozi na rufaa yake dhidi ya uamuzi huo kusikilizwa na Kamati Kuu ya Chadema.
Pia anataka Chadema iamuriwe kuitisha Baraza Kuu ili kujadili Rufaa hiyo,” anasema na kuongeza:
“Msingi wa madai ni kwamba wakati mchakato wa rufaa haujakamilika na wakati hajapewa nakala za mwenendo na uamuzi wa kumvua nafasi za uongozi, ameitwa na Kamati Kuu kujadiliwa kuhusu uanachama wake.
“Katika shauri dogo lililotolewa uamuzi mahakamani, mwombaji aliomba amri ya zuio ili Kamati Kuu au chombo kingine cha Chadema kisijadili uanachama wake mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu.”
Shauri hilo lilifunguliwa Januari 2 mwaka huu, siku ambayo mawakili Kibatala na Tundu Lissu wa Chadema walitoa mapingamizi dhidi ya maombi hayo na vifungu vya sheria ambavyo havikuwa sawa. 
Hoja za kinaLissu zilisema, hati ya kiapo ina upungufu na mahakama haina mamlaka kujadili migogoro ya vyama vya siasa na taasisi zenye tabia ya uhiari. Mahakama ilikataa mapingamizi yao yote.
“Wakati wa usikilizaji, Mahakama yenyewe (suo mottu) ikazitaka pande zote ziieleze Mahakama Kuu iwapo ni sahihi wakili kula kiapo kwa niaba ya mteja katika shauri kama lile. Pande zote ziliileza Mahakama kwamba ni sahihi, ingawa Wakili Msando alipinga aya ya nne ya hati ya kiapo kwa sababu za kisheria.
Anaendelea kusema kuwa hoja zao zilisisitiza kuwa  mwombaji amepewa nafasi ya kusikilizwa kwa kuitwa Kamati Kuu, na kwamba Mahakama haina mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya taasisi kama vyama vya siasa.

Baada ya kushinda katika pingamizi lake la kuikataza Kamati Kuu kutomjadili wala kumvua uanachama wake, sasa Zitto anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake mwezi ujao ili iwapo atashinda rufaa yake isikilizwe na Baraza Kuu la Chadema badala ya Kamati Kuu na hayo ndiyo majaliwa yake.
Inavyoonekana, ana imani na wajumbe wa Baraza Kuu kuliko Kamati Kuu. Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema Ibara ya 7.7.11 Wajumbe wa Baraza Kuu ni pamoja na wajumbe wote wa Kamati Kuu, Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, mikoa na wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu Mkuu na kuidhinishwa na Baraza Kuu.

Wengine ni wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne kutoka Bara na mmoja kutoka Zanzibar kwa kila Baraza.
Wengine ni wenyeviti wa wilaya za chama na mwakilishi wa jimbo na chama.  Hawa ndiyo watakaosikiliza na kuamua juu ya rufaa ya Zitto atakapoiwasilisha kwao. Je, atasalimika?
Hata kama Zitto atatimuliwa na Baraza hilo, bado anaweza kwenda mahakamani kupinga kutimuliwa, kama walivyofanya wabunge wenzake, David Kafulila aliyevuliwa uanachama na NCCR-Mageuzi na Hamad Rashid aliyetimuliwa CUF.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop