Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, February 17, 2014

KAULI YA RAIS KIKWETE KIZUNGUMKUTI KWA UPINZANI

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka wanachama, wadau na makada wa CCM, kuondokana na unyonge, imepokewa kwa hisia tofauti huku ikielezwa kuwa ni ya vitisho.
Juzi, wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala alisema: “Ni wakati wa kuacha unyonge na uvumilivu una kikomo chake.”
Alisema CCM inaingia kwenye uchaguzi huku ikishindana na wagomvi: “...Ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wao kufanya siasa,” alisema Kikwete bila kutaja jina la chama chochote cha siasa.
Alisema amechoshwa na vitendo vya ugomvi huku akitolea mfano wa tukio la Kahama mkoani Shinyanga ambako kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi na mwingine kumwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, mkoani Tabora.
Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete akisema: “Nimeipokea kwa mshtuko na ninawataka wafuasi wa chama changu kuwa watulivu na kuchukua tahadhari kubwa.”
“Nilichokifanya ni kuwaagiza wafuasi wa Chadema kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutolipiza kisasi ili kuhakikisha kwamba hakuna damu ya Mtanzania itakayomwagika Kalenga,” alisema.
Hatua ya Rais Kikwete, imekuja baada ya CCM kumtangaza, Godfrey Mgimwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga. Mgimwa ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha, hayati Dk William Mgimwa aliyefariki mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.
Mgombea huyo atachuana na mgombea wa Chadema, Grace Tengega.
Jana, Mbowe alisema ingawa Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM, alitakiwa kufahamu kwamba ni kiongozi wa nchi na ni Amiri Jeshi Mkuu ambaye vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo chini yake.
“Anapotoa kauli nzito kama hiyo, inatakiwa afahamu kwamba yeye si Mwenyekiti wa CCM tu, bali ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu, hakustahili kutoa kauli kama hiyo inayoweza kuamsha hisia,” alisema Mbowe.
Alisema kauli zake za kiitikadi za kupendelea chama chake wakati akifahamu kuwa yeye ni kiongozi wa Watanzania wote, zinawafanya wananchi wagawanyike kwa misingi ya vyama.
“Rais Kikwete anadai kwamba mtu wao alimwagiwa tindikali na mwingine kutolewa macho kwa bisibisi, lakini hazungumzii viongozi na wanachama wa Chadema waliouawa kwa kupigwa risasi na wengine kwa mabomu. Anasema hayo huku akifahamu fika kwamba kuna vyombo vya dola na Mahakama ambavyo vinashughulikia matukio hayo.”

Mbowe alidai kuwa Juni 15, 2013 wakati akifunga kampeni za udiwani mkoani Arusha, alirushiwa bomu la kivita na kusababisha vifo vya watu wanne lakini uongozi wa chama hicho ulipomwomba Rais aunde tume huru ya kimahakama hakuna kilichofanyika.
“Tumemwomba mara kadhaa Rais Kikwete kuunda tume huru ya kimahakama ili kuchunguza mauaji ya viongozi na wanachama wa Chadema ambayo yamekuwa yakitokea, lakini hakuna kilichofanyika,” alisema Mbowe ambaye ni pia kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
Alisema: “Rais Kikwete anasema wamekubaliana kwenye Halmashauri Kuu (ya CCM) kuacha unyonge, Halmashauri Kuu ina viongozi wote wakuu wa nchi, wanakubaliana kuwatenga wananchi kwa kufuata itikadi za chama chao, hii ni hatari.”
Mbowe alisema kauli ya Rais Kikwete inafanana na ile ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoitoa bungeni ya kuwataka askari polisi kuwapiga raia kwa wale wasiotaka kutii amri halali.

Akizungumzia kauli hiyo, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia alisema ameshtushwa na kauli ya Rais Kikwete na kumtaka kuitolea ufafanuzi ili kuondoa mgawanyiko katika jamii.
Alisema kauli ya ‘unyonge CCM sasa basi’ haikupaswa kutolewa naye hasa ikizingatiwa kwamba ndiye kiongozi mkuu wa nchi ambaye vyombo vya ulinzi na usalama viko chini yake.
“Ni kama amevielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kali dhidi ya vyama vingine vya siasa, ninamwomba alitolee ufafanuzi suala hili kabla halijaleta madhara kwenye jamii,” alisema Mbatia.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema kauli ya Kikwete inaashiria kuwa kutakuwa na matumizi makubwa ya vyombo vya dola katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga.
“Ninavyofahamu siyo kwamba anawaagiza wafuasi wa CCM kuacha unyonge na kuchukua hatua, bali anavielekeza vyombo vya dola kutumia nguvu kubwa zaidi,” alidai.
Mtatiro alisema anashangaa kauli ya namna hiyo kutolewa na Rais wakati ndiye anayetakiwa kuhubiri amani na kuvumiliana.

Akizungumza suala hilo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ali alisema wananchi wanatakiwa kuwa makini na kauli za wanasiasa zenye kujenga chuki.
“Vijana tusipigane kwa kugombanishwa na wanasiasa, tofauti zetu za kiitikadi zisitufanye tugombane kwani malengo ya wanasiasa ni kutoa kauli zenye utata kwa lengo la kupata kura, matatizo yetu yatuunganishe,” alisema Bashiru.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop