Friday, February 21, 2014

PADRE AFIA NYUMBA YA KULALA WAGENI, MCHUNGAJI AFIA NYUMBANI KWA MSHIRIKA WAKE

Mchungaji Geoffrey Maingi wa Kanisa la Redeemed Gospel aliyefia nyumbani kwa mshirika wake
Kiongozi wa Kanisa amekutwa akiwa amefariki dunia kwenye nyumba ya kulala wageni jijini Nairobi na kufanya vifo vya kutatanisha vya viongozi wa kidini kufikia wawili wiki hii.
Katika tukio la juzi, Padri wa Kanisa Katoliki, Otto Myer (70) ambaye ni raia wa Italia, alikutwa akiwa amefariki saa tano usiku chumbani mwake kwenye nyumba ya kulala wageni ya the Consolata huko Westlands, Nairobi.
Mwili wa padri huyo ulipatikana kwenye chumba hicho kando yake kukiwa na dawa, na baadhi ya jirani zake walisema alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mfupi.
Juzi, Mkuu wa Polisi Jimbo la Nairobi, Benson Kibue alisema maofisa wake wanachukulia kifo chake kuwa cha ghafla, hasa kutokana na kwamba amekuwa akiugua kwa siku kadhaa.
“Hatutaharakisha kusema kilichomuua. Kwa sasa tunajua hiki ni kifo cha ghafla, ikizingatiwa kuwa amekuwa akiugua. Upasuaji wa maiti ndio utakaoeleza zaidi kilichomfanya afariki,” akasema Kibue.
Lakini maofisa wa polisi waliofika mahali hapo pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa gesti hiyo ambao hawakutaka kutajwa, walisema kwamba chumbani alimokufa padri huyo mlikuwa na dawa pamoja na pombe.
Wakizungumza na waandishi wetu, walisema kwamba padri huyo alikuwa ameenda katika hospitali ya karibu kutafuta tiba siku ya Jumanne.

Kifo cha Padri Myer kilitokea saa chache baada ya kifo cha mchungaji Geoffrey Maingi wa Kanisa la Redeemed Gospel nyumbani kwa mmoja wa washirika wake katika Mtaa wa Buruburu, Nairobi.
Sawa na Padri Myer, Kasisi Maingi pia alikuwa na umri wa miaka 70 na pia alifariki dunia kwenye vyumba katika hali ya kutatanisha.
Kwenye kisa cha Buruburu, Kasisi Maingi  alisemekana kuegesha gari lake nje ya duka la jumla la Tuskys na kwenda nyumbani kwa mwanamke mshirika wa Kanisa lake, ambaye alikiri kuwa mbali na kuwa kiongozi wake wa kiroho, yeye pia alikuwa rafiki yake.
Mwanamke huyo alisema kuwa mchungaji huyo alikuwa nyumbani kwake kwa maombi. Tukio hilo lilishuhudiwa katika mtaa wa Buruburu mjini Nairobi Kenya.
Mwili wa Maingi, ulikutwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, baada ya kufariki kutokana na sababu ambazo hazijulikani.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About