Mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Wananchi
wanne kati ya watano wanaamini kuwa mafuta na gesi yatawanufaisha wao,
watoto wao na nchi yao kwa ujumla. Wakati huo huo, wananchi wanne kati
ya kumi (37%) wanaamini kuwa viongozi wa Serikali na matajiri ndio
wataofaidika zaidi. Pia, zaidi ya nusu (55%) wangependa baadhi ya
mapato ya mafuta na gesi wapewe wananchi moja kwa moja kama fedha
taslimu.
Matokeo
haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la
Kusimamia Maliasili: Wananchi wanasemaje? Utafiti huu ulifanywa kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia na umetokana na takwimu za Sauti za
Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu ya mkononi wenye
uwakilishi wa kitaifa.
Utafiti
unaonesha kwamba matakwa ya wananchi ni kuwa, angalau kiasi cha mapato
ya mafuta na gesi kipelekwe moja kwa moja kwa wananchi. Mwananchi mmoja
kati ya watano (20%) angependelea kiasi kikubwa cha fedha kipelekwa moja
kwa moja kwa wananchi; wakati wananchi asilimia 18 wangependelea kuwe
na mgawo sawa wa mapato kati ya serikali na wananchi. Asilimia 17
wangependelea Serikali ipate asilimia kubwa zaidi ya mapato kwa ajili ya
kuendeleza miundombinu na huduma za kijamii na wananchi wapewe kiasi
kinachobaki.
Hata
hivyo, Watanzania walio wengi (43%) wangependa mapato yote yaende
Serikalini kwa ajili ya kugharamia huduma muhimu. Isitoshe, wananchi
walipoulizwa namna wanavyoamini mapato ya rasilimali yanaweza kuleta
manufaa kwa Watanzania, nusu yao (46%) walisema mapato yatumike katika
kutoa huduma za afya na elimu, na wananchi wanne kati ya kumi (20%)
walipendekeza yatumike kwenye miundombinu au kwenye mipango ya kupambana
na umaskini (17%).
Linapokuja
suala la usimamizi wa maliasili, jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa
Tanzania haiangukii kwenye uhanga wa laana ya utajiri wa maliasili.
Uzoefu kutoka nchi nyingine unaonyesha kuwepo kwa uwazi kuhusu mapato na
mchakato kama kitu muhimu sana katika kuepuka laana hii, pamoja na
ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi yanayohusu namna mapato
yanavyosimamiwa.
Hivi
sasa, ingawa Watanzania wengi (64%) wanafahamu ugunduzi wa mafuta na
gesi, Utafiti wa Sauti za Wananchi ulibaini kuwa Watanzania wawili kati
ya watatu (65%) wangependa kupata taarifa zaidi. Pindi taarifa
zinapokosekana, tetesi na uvumi mara nyingi huziba pengo hilo. Ingawa
makadirio ya sasa yanasema kuwa uchimbaji mkubwa wa mafuta na gesi
hautaleta faida katika kipindi cha miaka saba hadi kumi ijayo, mwananchi
mmoja kati ya watatu (36%) anaamini kuwa makampuni ya mafuta na gesi
tayari yameshaanza kupata fedha kutokana na ugunduzi huu. Isitoshe
wananchi watatu kati ya kumi (28%) hawana uhakika kama tayari kuna
mapato kutoka kwenye mafuta na gesi au la. Aina hii ya mapengo kati ya
mitazamo na uhalisia, kama haitaangaliwa vizuri, inaweza kusababisha
wananchi kutoridhishwa na usimamizi wa maliasili.
Mjadala
mwingine mkali umekuwa juu ya nafasi ya makampuni ya ndani na ya nje ya
nchi katika kuchimba mafuta na gesi. Wafabiashara wengi wamedai kwa
msisitizo upendeleo utolewe kwa makampuni ya Tanzania. Nusu ya
Watanzania (52%) wangependa kunufaika na utaalamu wa makampuni ya kigeni
katika sekta hii, lakini kwa kushirikiana na makampuni ya ndani ambayo
yanapaswa kumiliki hisa kubwa zaidi katika ushirikiano wa kibiashara
hio. Mwananchi mmoja kati ya watatu (35%) anaamini kuwa makampuni ya
ndani yapewe kipaumbele kwenye zabuni za makubaliano. Aidha, Watanzania
sita kati ya kumi (61%) wako tayari kuona mafuta na gesi yakiuzwa
kimataifa kwenye nchi zote. Hata hivyo, wananchi watatu kati ya kumi
(28%) wanafikiri gesi inapaswa kutumika nchini tu, na mwananchi mmoja tu
kati ya ishirini (5%) anafikiri mauzo ya gesi yafanyike nchi za Afrika
Mashariki pekee.
Rakesh
Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema “Kama tunataka watu wa Tanzania
wanufaike na ugunduzi wa gesi, tunahitaji uongozi wa serikali ulio
imara, wenye uwazi na ubunifu. Kuwepo kwa mfuko huru wa utajiri wa taifa
ni sehemu moja muhimu ya ufumbuzi. Hata hivyo, tunahitaji kufikiria juu
ya njia mbadala, kama vile kupeleka fedha moja kwa moja kwa watu. Jambo
la msingi zaidi ni kuweka wazi taarifa, kusikiliza maoni ya wananchi na
kuwasiliana ili kujenga imani ya wananchi kufahamu namna fedha za gesi
inavyotumika.”
0 comments:
Post a Comment