Tapeli
lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka
washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya
kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari
wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma-
Ledama.
Kwa
mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo
alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema
wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo
wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na
kung’oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.
“wakasema
fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2
wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa
laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine
wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa
kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.
Na
kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange.
tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu
wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo
havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka
tuite Polisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano
waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme,
nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka
Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani,
tukawakuta wameondoka.
Mzee
akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City,
tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo,
tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
0 comments:
Post a Comment