Moto mkubwa umetokea ktk msikiti wa Mtambani uliopo endeo la Kinondoni "B" na kuunguza eneo lote la juu la msikiti huo ambako kunasadikiwa kulikua na madarasa kwa ajili ya shule inayomilikiwa na msikiti huo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ila inasemekana ulianza ktk chumba kimoja walichokua wanalala wanafunzi wa shule hiyo baadhi wa kike na inasemekana huenda ikawa ni mshumaa ndio ulisababisha moto huo lakini hizi ni tetesi kwa baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo na tunangojea taarifa maalumu kutoka kwa kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni kuthibitisha chanzo cha moto huo. Endelea kutufuatili zaidi kupata taarifa yote ya tukio hili
No comments:
Post a Comment