Rais Barrack Obama wa Marekani
ametoa wito kwa rais wa Rwanda Paul Kagame, kusitisha msaada anaotoa kwa
makundi ya waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kwa mujibu wa ikulu ya White House, rais Obama
alifanya mazungumzo ya simu ya Rais Paul Kagame siku ya jumanne, ambapo
aliafiki tangazo lake la kujitolea katika harakati za kupatikana kwa
amani katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.Waasi wa M-23 wapo katika eneo la mashariki mwa Congo licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa kutunza amani wa umoja wa mataifa katika eneo hilo.
Ripoti ya hivi majuzi iliyochapishwa na Umoja wa Mataifa iliishutumu serikali ya Rwanda kwa kutoa msaada kwa waasi hao wa Congo, madai ambayo serikali ya Rwanda Imekanusha vikali.
0 comments:
Post a Comment