Mji wa Mecca nchini Saudi Arabia
Wizara ya mambo ya ndani nchini Saudi Arabia, imesema kuwa raia mmoja wa Sudan amenyongwa kwa kukatwa kichwa.
Kwa mujibu wa tangazo kutoka kwa wizara hiyo,
iliyochapishwa na shirika la habari la serikali, Othman Mohammed
alinyongwa katika mji wa Magharibi wa Mecca.Mohammed alipatikana na hatia ya kumuua raia mwingine kutoka Sudan, Salah Ahmed kwa kumpiga vibaya kichwani.
Chini ya sheria kali katika Ufalme huo wa Kiarabu, adhabu ya kifo hutolewa kwa makosa kadhaa, yakiwemo mauaji, ubakaji na ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Shirika la kutetea haki za kibinadam la Amnesty International limesema kuwa watu 89 walinyongwa nchini Saudi Arabia mwaka uliopita pekee.
0 comments:
Post a Comment