Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela, ameruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali moja mjini Pretoria.
Ikulu ya rais nchini humo imesema rais huyo wa zamani wa Afrika kusini, anaendelea kupata nafuu nyumbani mwake.Msemaji wa serikali amesema Mandela bado hajapoa kabisa na ataendelea kupokea matibabu nyumbani mwake mjini Johannesburg.
Mandela alilazwa hospitaini siku kumi na nane zilizopita kufuatia maambukizi ya mapafu
Mkewe Graca Machel, na rais Jacob Zuma walimtembelea Bwana Mandela siku ya Krismasi na walisema kuwa alikuwa katika hali nzuri.
Baada ya ziara hiyo, rais Zuma alisema kuwa madaktari wamefurahishwa na jinsi Bwana Mandela alivyokuwa akiendelea kupona kwa hara licha ya umri wake.
Rais Zuma aliwashukuru raia wa nchi hiyo kwa risala zao za heri njema kwa rais huyo wa zamani.
Hata hivyo aliomba raia na waandishi wa haabri kuwa na subira na wakati huo huo kuwapa bwana mandela na familia yake nafasi wanayohitaji.
Hi ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo rais Mandela amelazwa hospitalini kwa muda mrefu zaidi.
Mjuu wa Bwana Mandela, Mandla, amesema, kutokuwepo kwa babu yao wakati wa Krismasi kumewasikitisha sana kwa sababu hawakudhani kuwa angesalia hospitalini kwa muda huo wote.
0 comments:
Post a Comment