Itakuwa ni faraja iliyoje sababu tuna imani kwamba kutokana na uwezo wa kifedha na ubunifu mkubwa katika bidhaa na biashara mbali mbali kampuni hii ya mabasi itakuwa na magari ya kisasa na yenye viwango vya juu.
Nadhani wote tunashuhudia jinsi mabasi mengi ambayo tunapanda yasivyo na
viwango na kusababisha ajali za mara kwa mara ukiachilia mbali uzembe
wa madereva, viwango vya magari navyo huchangia ajali. Mfano mengi
yameundwa kwa chassis za malori ambapo hazi kuundwa mahsusi kwa ajili ya
kubeba abiria. Pia watoaji huduma wengi wamekuwa ni wababaishaji.
Zaidi wengi tunajua jinsi biashara hii ya ma bus inavyo milikiwa kwa
kiwango kikubwa na wana siasa. Kwa hiyo tunaomba katika hili ushindani
uwe wa kweli. Boresheni huduma zenu ili kuweza kumkabili Bakhresa. Sote
tuna kumbuka treni la Mwakyembe lilivyoanza kuletewa mizengwe na wakubwa
hawa wanaomiliki madaladala kabla ya umma kuingilia kwa nguvu kupinga
hujuma zozote.
0 comments:
Post a Comment