Orodha ya jarida la Forbes la watu 40 matajiri zaidi barani Afrika imetupa jibu la ‘uhakika’ nani ni mtu tajiri zaidi kuliko wote nchini Tanzania. Si mwingine zaidi ya Said Salim Bakhresa ambaye amekamata nafasi ya 30 kati ya matajiri 40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 520 hadi kufikia November, 2012.
Bakhresa ana historia ya pekee kwa kuacha shule akiwa na miaka 14 na kujiingiza kwenye biashara ndogo ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na biashara ya unga wa kusaga. Leo hii Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu 2,000 na ni kampuni kubwa zaidi Tanzania. Bidhaa zake zina umaarufu mno nchini na nje ya nchi ambazo ni pamoja na unga, vinywaji, ice cream, usafiri wa meli na mafuta miongoni mwa nyingine.
Kampuni ya Bakhresa ni wazalishaji wakubwa zaidi wa unga wa ngano Afrika Mashariki na kati ambayo huzalisha kiasi cha 3,200 za tani za metric. Kampuni yake huendeshwa na wanae wa kiume waliogawana vitengo mbalimbali.
Kwa kuona matajiri wote Africa fuata link hii Africa-billionaires list
0 comments:
Post a Comment