WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru Kawambwa leo ametangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la
Saba 2012 uliofanyika nchini kote tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.
Katika Mtihani huo Jumla ya wanafunzi
894,881 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambapo wavulana ni 426,285
sawa na asilimia 47.64 na wasichana ni 468,596 sawa na asilimia 52.36.
Aidha, kati ya wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379 ambao
walitarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi
20,502 walitarajiwa kufanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo
waliyoitumia kujifunzia.
Wanafunzi wasioona waliosajiliwa
kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39. Watahiniwa
wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao
wavulana ni 238 na wasichana ni 257.
0 comments:
Post a Comment