Takriban watu 39 wameuawa na
wengi kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka upya katika eneo la Tana
River, nchini Kenya baada ya wavamizi wasiojulikana kushambulia kijiji
cha Kipao alfajiri ya leo.
Polisi wamethibitisha hayo na kusema huenda idadi hiyo ikaongezeka.Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na watu kutoka kwa jamii ya Pokomo katika kijiji ch Kipao dhidi ya watu wa Kabila la Ormo.
Nyumba kadhaa zimeripotiwa kuteketezwa na watu kadhaa kujeruhiwa kwa kukatwa kwa mapanga.
Mapema mwezi wa Agosti na Septemba, Eneo la Tana River katika pwani ya Kenya lilikumbwa na mapigano ya kikabila yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja, wakiwemo maafisa kadhaa wa Polisi.
Idara ya polisi imesema watu kutoka kwa jamii hizo mbili walipoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa wakiwemo watoto na wanawake.
Haki za malisho
Shirika la msalaba mwekundu limesema takriban watu 30 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa vibaya, akiwemo mtoto wa umri wa mwaka mmoja.
Aidha shirika hilo linasema nyumba 40 ilichomwa na wavamizi hao.
Maafisa wa wa shirika hilo la msalaba mwekundu wanaendelea na msako katika eneo hilo kuwatafuta miili zaidi.
Maafisa zaidi wa polisi na maafisa wa kutoa misaada ya dharura wamepelekwa katika eneo hilo kwa ndege ili hali wale waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali kuu ya mkuu mjini Mombasa.
Mwezi Agosti mwaka huu, jamii hizo mbili zilizzozana baada ya wakulima kutoka kwa jamii ya Ormo kupeleka mifugo wao katika ardhi inayodaiwa kumilikiwa na watu wa jamii ya Pokomo.
Polisi wamekuwa katika eneo hilo kujaribu kuwapokonya silaha makundi hayo mawili.
Wakaazi wa eneo hilo wanasema uhasama kati ya jamii hizo mbili umekuwa ukitokota katika siku za hivi karibu
0 comments:
Post a Comment