Askari wa upelelezi akifanya vipimo eneo la tukio.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug).
Baba
mzazi wa mtu aliyejulikana kama Robert Karamagi ambaye alifariki
kutokana na majeraha ya kuungua kwa moto kwa kile kinachoaminika
kuchomwa kwa makusudi ndani ya nyumba ya mwanamuziki Jose Chameleone wa
Uganda ameibuka na kusema mtoto wake hakujilipua mwenyewe kama
inavyodaiwa.
Karamagi aliyekuwa na umri wa miaka 27 alifariki katika hospitali ya Mulago saa chache baada ya kufikishwa hapo na kulazwa.
Matukio
yaliyosababisha Karamagi aliyevamia nyumba ya msanii huyo kukumbwa na
mkasa huo bado ni kitendawili huko mke wa Chameleone Bi. Daniella
akisisitiza kuwa Karamagi alijitia moto mwenyewe alipotaka kujaribi
kumchoma bibie huyo.
Askari
wa jeshi la polisi Uganda wakifanya mahojiano na Jose Chameleone (wa
pili kushoto) nje ya nyumba yake.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug).
Lakini baba wa mtu huyo Meja Benedict Kyamanywa amepingana na ripoti kuwa mwanawe alijichoma moto mwenyewe. Amesisitiza kuwa mwanaye alifungwa kwa kamba na kuchomwa moto ndani ya makazi ya mwanamuziki huyo.
Ameongoza kuwa kabla mwanaye huyo hajakata roho alimuambia kuwa alifungwa kamba na kuchomwa na mafuta ya ndege.
Hata
hivyo katika hatua nyingine Meja Kyamanywa ambaye ni daktari msaidizi
wa Kakiri Barracks amesema kuwa mtoto wa alikuwa na matatizo ya akili,
na kuwa kijiji kizima kilikuwa kinajua akiwemo Chameleone mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment