Washukiwa wa kundi la wapiganaji
wa kiisilamu , wamelaumiwa kwa mauaji ya watu 23 katika mashambulizi
tofauti Kaskazini mwa Nigeria.
Walio shuhudia mauaji hayo wanasema kuwa
washambuliaji waliwalenga watu waliokuwa wanauza nyama ya wanyamapori,
katika eneo la Damboa siku ya Jumatatu na kuwaua watu 18.Watu wengine watano walifariki Jumanne wakati kundi la wanaume waliokuwa wanacheza mchezo wa kamari walishambuliwa mjini Kano.
Kundi la Boko Haram, linalopigana kutaka kuweka sheria za kiisilamu, nchini Nigeria limekuwa likifanya mashambulizi, katika sehemu kadhaa nchini humo.
Boko Haram imelaumiwa kwa vifo vya takriban watu 1,400, Kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka 2010. Mwaka jana pekee , kundi hilo lilihusishwa na vifo vya watu 600.
Siku ya Jumatatu, watu waliokuwa wamejihami, walifyatulia risasi katika soko moja jimbo la Borno , wakiwalenga watu waliokuwa wanauza nyama ya nyani, na nguruwe.
"watu waliokuwa wamejihami, na wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram, walikuja katika soko moja eneo hilo, na kuwapiga risasi watu 13, papo hapo na wengine watano walifariki kutokana na majereha yao.'' alisema afisaa mmoja.
Eneo la Damboa liko karibu na hospitali moja mjini Borno katika jimbo la Maiduguri, ngome ya Boko Haram.Kundi hilo liliundwa mjini humo mwaka 2002.
Wakati huohuo, ripoti zinasema kuwa shambulizi lengine baya sana limefanywa mjini Kano , mji mkuu Kaskazini mwa Nigeria,umbali wa kilomita 500, Magharibi mwa Damboa.
Watu waliokuwa wanaendesha pikipiki waliwanywaftulia risasi, vijana waliokuwa wanacheza nje , kwa mujibu wa taarifa za polisi.
Mchezo wa kamari pia umeharamishwa katika dini ya kiisilamu.
0 comments:
Post a Comment