Hali yawa tete kwa serikali ya Ufaransa nchini Mali. Serikali ya Uingereza inatarajiwa kujadili mpango wa kutoa msaada zaidi
kwa wanajeshi wa Ufaransa wanaopambana na waasi nchini Mali.
Serikali ya Uingereza
inatarajiwa kujadili mpango wa kutoa msaada zaidi kwa wanajeshi wa
Ufaransa wanaopambana na waasi nchini Mali.
Waziri mkuu David Cameron, amesema kuwa huenda
msaada za usafiri na kijasusi ukatolewa kwa wanajeshi hao. Ndege mbili
za kijeshi tayari zimetolewa kwa jeshi la Ufaransa.Waziri wa ulinzi anasema kuwa hakuna mipango ya kufanya mashambuli ya ardhini kwa sasa.
Kuhusu vifo vya raia wa Uingereza katika mashambulizi kwenye kiwanda cha gesi nchini Algeria yaliyofanywa na wapiganaji wa kiisilamu, bwana Cameron alisema kuwa eneo la Kaskazini mwa Afrika linageuka kuwa ngome ya wapiganaji wa kiisilamu.
Wasiwasi kuhusu athari za kundi la kigaidi la al-Qaeda katika ukanda huo, zinaonekana kudhibitiwa kufuatia mpango wa kuwapeleka wanajeshi wa Ufaransa kupambana na wapiganai wenye uhusiano na Al Qaeeda nchini Mali na Algeria ambako waliwateka nyara wafanyakazi wa kigeni.
Wanamgambo waliowashambulia wafanyakazi wa kigeni nchini Algeria, ambapo takriban mateka 48 waliuawa wametoa wito kwa Ufaransa kusitisha harakati zao nchini Mali.
Jibu la jamii ya kimataifa kwa tisho hili liitakuwa swala muhimu katika ajenda ya mkutano wa nchi nane zilizostawi duniani G8.
"lazima tupambane na hao magaidi kwa kutumia mbinu zote za kuweka usalama. Lazima tuwakomeshe, kijeshi. Ni lazima tuzungumzie hii kasumba yao, sharti tufunge hii nafasi wanayoitumia, kuendesha harakati,zao'' alisema waziri mkuu.
0 comments:
Post a Comment