Askari wa kutuliza ghasia wakijiandaa kuzuia vurugu
zilizotokea Mtwara, leo kwa kile kilinachodaiwa ni mwendelezo wa vurugu
za madai ya gesi.
Katika vurugu hizo, mwandishi wa habari wa Chanel Ten, amejeruhiwa kichwani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu, huku ikielezwa kuwa watu hao wamevamia Nyumba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, na kuipiga mawe na kuvunjwa vioo na kuchomwa moto.
Aidha imeelezwa kua katika harakati hizo pia Mahakama ya Mwanzo imechomwa moto na kusababisha askari kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao na kulazimika Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, kuingilia kati kutuliza ghasia hizo.
Eee,Mungu tunakuomba uiponye inchi yetu ya Tanzania. Tupatie amani, utulivu, upendo na mshikamano. Amen
ReplyDelete