Basi
la Abiria la Kampuni ya Burudani linavyoonekana baada ya kupata ajali
mbaya sana leo iliyopelekea kupoteza maisha kwa watu 12 huku wengine
zaidi ya 30 wakiwa kwenye hali mbaya.ajali hiyo imetokea leo eneo la Kwaluguru,Kwedizinga wilayani Handeni,Mkoani Tanga.
Watu
12 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya
basi la abiria walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Burudani linalofanya
safari zake kati ya Korogwe mkoani Tanga kwenda Jijini Dar es Salaam
kuacha njia na kupinduka.
Ajali hiyo imetokea mapema leo asubuhi majira ya saa 1.30 katika eneo la Kwaluguru,Kwedizinga wilayani Handeni,Mkoani Tanga.
Akithibitisha
kutokea ajali hiyo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Constantine Massawe
alisema kuwa ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T 610
ATR aina ya Nissan,imetokea leo na kusababisha vifo vya abiria 12 na
wengine zaidi ya 30 wako kwenye hospitali ya Wilaya ya
Korogwe,wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda
Massawe aliendelea kusema kuwa dereva wa basi hilo ajulikanaye kwa
jina la Luta Mpenda(35) ni miongoni mwa watu wanaosadikiwa kufa na
kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya
Korogwe ya Magunga.
“Majeruhi
wamekimbizwa katika hospitali ya magunga na hali zao bado siyo nzuri
sana lakini na miili ya marehemu pia imehifadhiwa magunga”,alisema
Kamanda Massawe.
Hata
hivyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa
basi hilo ambapo alipofika kwenye kona ya eneo la Kwalaguru gari
lilimshinda na kupinduka.
Wakazi wa Wilaya ya Korogwe wakiwa wamefurika kwenye Hospitali ya Magunga walipohifadhiwa marehemu na majeruhi.
Wauguzi wa Hospitali ya Magunga wakiendelea kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo akitokea chumba cha maiti cha Hospitali hiyo.
0 comments:
Post a Comment