Mkurugenzi
Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akikata utepe kuashiria
ufunguzi rasmi wa makao makuu ya ofisi za Azamtv, yaliyopo barabara ya
Nyerere, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam
Media Ltd. Rhys Torrington akishuhudia tukio hilo.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa akizungumza na waandishi
wa habari baada ya uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Ofisi za Azam
TV na kusisitiza umuhimu wa kupanua wigo wa upatikanaji wa Chaneli zao
50 na kutoa huduma bora zenye ubora wa hali ya juu katika kuwafikia
wateja wote wa ndani na nje ya nchi.
AzamTV leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Huduma
za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa
Desemba 6, 2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenye kisimbuzi
kungalia bure hadi hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa
ada ya shilingi 12,500 kwa mwezi.
Kwa
kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli
maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu
za Azam ambazo ni:
-Azam One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa lugha ya Kiswahili.
-Azam Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
-SinemaZetu – Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Kwa pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya michezo, tamthilia, watoto na maisha.
Ofisi imefunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Ltd.
“Ofisi
hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia
thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya
utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu
kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika.
Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema
Bakhresa
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington, akisisitiza
upatikanaji wa vinga’muzi vya Azamtv kwamba vitapatikana maeneo karibu
yote ya Tanzania Bara na Visiwani kwa manufaa ya watanzania wote.
Rhys
Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona
faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV ipo sokoni kwa ajili ya kila
mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu
kote nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – si tu katika ofisi
hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50
katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”
Azam
Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia
kampuni yake tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji
wa vipindi wa hapa Tanzania.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akionyesha cake maalum
iliyoandikwa “Azam Tv” ikiwa ni mbwembwe za kusherehesha uzinduzi
wa makao makuu ya ofisi za Azamtv, yaliyopo barabara ya Nyerere, jijini
Dar es Salaam.
Wageni
waalikwa wakijisevia cake mara baada ya uzinduzi rasmi wa Ofisi za Azam
Tv ziliyopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akisalimiana na baadhi
ya wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria uzinduzi huo leo jijini Dar.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd. Rhys Torrington, akisalimiana na
wasanii wakongwe wa Bongo Movie kwenye sherehe za uzinduzi wa Ofisi za
Azamtv uliofanyika leo jijini Dar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Azam Media Ltd. Bw. Yusuf Bakhresa, akibadilishana mawazo
na mmoja wa wadau ambaye alimpongeza kwa hatua nzuri ya kuleta mapinduzi
kwenye ulimwengu wa Digitali.
Dr.
Cheni akibadilishana mawazo na msanii mwenzake wa Bongo Movie Natasha,
huku Msanii Batuli akishow love
Wasanii
wa Bongo Movie katika picha ya pamoja huku nyuso zao zikiwa zimejaa
furaha tele mara baada ya kuzinduliwa kwa Ofisi za Azamtv zilizopo
barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Msanii Monalisa na Batuli
Wafanyakazi
wa Azamtv kitengo cha Huduma kwa wateja wakiwa tayari kuwahudumia
wateja wao walionaza kumiminika kwenye makao makuu ya Ofisi mpya za
Azamtv zilizopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wakiwa wamejipumzisha kwenye Ofisi za Azamtv kusubiri kupewa huduma.
Vijana watanashati na nadhifu wakiwa tayari kuwahudumia wateja wao.
Mdau Othman Michuzi (kushoto) akipewa maelezo ya Chaneli mbalimbali zaidi ya 50 zinazopatikana kwenye King’amuzi cha Azamtv.
0 comments:
Post a Comment