Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kusimama njiani akitokea wilayani
Makete akielekea wilayani Wanging”ombe, katika ziara yake maalum ya Mkoa
wa Njombe kuhusu Chama cha Mapinduzi kilivyopokea kifo cha mpigania
uhuru wa Afrika Kusini na mtu aliyeheshimiwa sana duniani Mzee Nelson
Mandela kama alivyojulikana kama “Madiba” aliyefariki dunia usiku wa
kuamkia Ijumaa tarehe 6, Kinana amesema CCM inatambua jinsi Nelson
Mandela alivyoipigania nchi yake na Afrika kwa ujumla, kuikomboa
mikononi mwa ubaguzi wa rangi na kuiweka huru, Ameongeza kwamba CCM na
wanachama wake pamoja na watanzania wote watakumbuka mambo mema yote
aliyoifanyia nchi yake na Afrika kwa ujumla na kuyaenzi kwa vitendo.
Katibu Mkuu wa Cchama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kukagua shule ya sekondari ya Makete Girls iliyopo katika kijiji cha Mtweve wilayani Makete leo akiwa njiani kwenda Wilayani Wanging”ombe, kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kukagua sekondari ya Makete Girls katika kijiji cha Mtweve akiwa njiani kwenda Wanging”ombe mkoani Njombe, Kutoka kulia ni Toto Timoth ambaye ametoa tani tano ya mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo,Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa
na Uhusiano wa Kimataifa
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akiongozana Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa wa Njombe mara baada ya magari kukwama njiani kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa wa Njombe wakisubiri magari yaliyokuwa yamenasa kwenye tope wakati msafara ukielekea wilayani Wanging’ombe leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kutoka kulia na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wa pili pamoja na waandishi wahabari wakitembea kwa miguu huku magari yakiwafuata mara baada ya kuyanasua kwenye tope.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Bi.Esterina Kilasi akimkaribisha Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili
wilayani Wanging’ombe leo, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni
Mstaafu Aseri Msangi.
“Kweli Bibi ana Huruma” Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
Bibi Geremana Mrwiro mwanakijiji ambaye alileta jembe ili litumike kwa
kusaidia kunasua magari yaliyokuwa yamekwama kwenye tope
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza katika kijiji cha Usuka kilipo kituo cha
Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima wilayani Wanging’ombe ambapo
Katibu mkuu wa CCM alitembelea vijana walioamua kujiunga pamoja na
kuendesha kilimo .
Baadhi ya vijana hao wakinyanyua kadi zao juu ili kula kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi kijana Said Mkweta.
Utulivu wa kula kiapo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo
kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi kuhuso
moja ya Power Tiller itakayotumiwa na vijana hao kulimia shamba lao ili
kuwahi mvua zinazonyesha. Gari lililokuwa likitumiwa na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa likinasuliwa kwenye tope mara baada ya kuteleza na kuingia kandokando ya mtari
Juhudi za kunasua zikiendelea.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata kulia Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kushoto na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakitoka nje mara baada
ya katibu mkuu huyo kuzindua jengo la kitegauchumi la CCM mkoa wa Njombe
leo ambalo limepangishwa na Wizara ya Fedha.
0 comments:
Post a Comment