Welcome to our online store Portal

Template Information

New Products
Showing posts with label Kinana. Show all posts
Showing posts with label Kinana. Show all posts

Tuesday, December 10, 2013

KINANA ATUMIA TRENI KUSAFIRI KUTOKEA MAKAMBAKO KUELEKEA DAR

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akipanda behewa na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam, saa 12, 30,  Desemba 9, 2013,  kwa  treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 22, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana saa 2.30 asubuhi.
2. Kinana, Migiro na Nape kwenye Treni Mlimba 2
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishuka kwenye behewa  na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), kukagua stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro, wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam, saa 12, 30,  Desemba 9, 2013,  kwa  teni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 22, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana saa 2.30 asubuhi.
 Dk. Asha-Rose Migiro na Nape wakishuka kwenye treni katika stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa na Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Mlimba wilayani Kilombero mkoani Morogoro, Selemani Balali (kulia) aliposhuka na msafara wake, kwenye stesheni ya Mlimba, akiwa njiani kutoka Makambako kwenda Dar es Salaam, jana
 Kinana na msafara wake, wakiwa na viongozi wa Kata ya Mlimba, alipokwenda kukagua stesheni ya eneo hilo. Mbele ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
 Kinana, Dk. Asha-Rose Migiro na Nape Nnauye wakitoka kukagua jengo la stesheni ya Mlimba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua karanga  kwa mwananchi aliyekuwa akifanya biashara ya karanga hizo kwemye stesheni ya Mlimba, Wilayani Kilombelo mkoani Morogoro
 Kinana akimlipa fedha muuzaji huyo wa karanga, Josephine  Amani
 Kinana akiuliza bei ya embe zilizkuwa zinauzwa na mwananchi kwenye stesheni ya Mlimba
 Kinana na Nape wakiuliza bei ya samaki kwa muuzaji wa bidhaa hiyo kwenye stesheni ya Mlimba, jana
 Dk. Asha-Rose Migiro na Nape wakitazama samaki waliokuwa wanauzwa kwenye stesheni ya Mlimba
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga stori na baadhi ya wasafiri kwenye stesheni ya Mlimba.
 Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na mmoja wa viongozi wa CCM waliompokea Kinana na msafara wake kwenye stesheni ya Mlimba
 Abiria akipitisha mtoto dirishani wakati treni inatoka Makambako
 Treni ikichana msitu kwenda Dar es Salaam
Treni ikipita katika ‘tanuru’ ndani ya mlima wakati ikitoka Makambako kwenda Dar es Salaam
MAPOKEZI DAR
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Madabida akimlaki Kinana kwenye stesheni ya TAZARA baada ya Kinana na msafara wake kuwasili Dar es Salaam leo asubuhi. Anayeshuka nyuma ni Dk. Asha-Rose Migiro.
 Kinana akiwa naNape, Dk. Asha-Rose na Madabida wakati akipita katika paredi la mapokezi la UVCCM, stesheni ya TAZARA
 Kinana na Nape wakiagana kwa furaha na waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wote, baada ya kuwasili stesheni ya TAZARA Dar es Salaam, leo asubuhi
 Kinana akimsalimia Kaimu Mkurugenzi wa UHURU FM, Angel Akilimali kwenye mapokezi hayo
 Kinana akisalimiana na Mbunge wa Temeke, Abbasi Mtemvu kwenye stesheni hiyo. Badaye Kinana alizungumza na wananchi waliofika kwenye mapokezi hao ambapo aliwashukuru sana kwa mapokezi huku akieleza kwamba WanaCCM aliokutana nao kwenyeziara yote wamemtia moyo wa kuendelea na ziara nyingine ya aina hiyo katika mikoa mingine.
View detail

Saturday, December 7, 2013

KINANA AKATISHA KWA MUDA ZIARA YAKE KUOMBOLEZA KIFO CHA MANDELA AKI


1b
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusimama njiani akitokea wilayani Makete akielekea wilayani Wanging”ombe, katika ziara yake maalum ya Mkoa wa Njombe kuhusu Chama cha Mapinduzi kilivyopokea kifo cha mpigania uhuru wa Afrika Kusini na mtu aliyeheshimiwa sana duniani Mzee Nelson Mandela kama alivyojulikana kama “Madiba” aliyefariki dunia usiku wa kuamkia  Ijumaa tarehe 6, Kinana amesema CCM inatambua jinsi Nelson Mandela alivyoipigania nchi yake na Afrika kwa ujumla, kuikomboa mikononi mwa ubaguzi wa rangi na kuiweka huru, Ameongeza kwamba CCM na wanachama wake pamoja na watanzania wote watakumbuka mambo mema yote aliyoifanyia nchi yake na Afrika kwa ujumla na kuyaenzi kwa vitendo.
2a2
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akizungumza nao alipozungumzia kifo cha ayati Nelson Mandela huko Wanging”ombe mkoani Njombe leo.
2
Katibu Mkuu wa Cchama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kukagua shule ya sekondari ya Makete Girls iliyopo katika kijiji cha Mtweve wilayani Makete leo akiwa njiani kwenda Wilayani Wanging”ombe, kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro. 1a
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephin Matiro akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kukagua sekondari ya Makete Girls katika kijiji cha Mtweve akiwa njiani kwenda Wanging”ombe mkoani Njombe, Kutoka kulia ni Toto Timoth ambaye ametoa tani tano ya mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo,Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa
 na Uhusiano wa Kimataifa
5
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akiongozana Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa wa Njombe mara baada ya magari kukwama njiani kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha 6
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Hosea Mpagike Katibu wa CCM mkoa wa Njombe wakisubiri magari yaliyokuwa yamenasa kwenye tope wakati msafara ukielekea wilayani Wanging’ombe leo. 7
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kutoka kulia na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wa pili pamoja na waandishi wahabari wakitembea kwa miguu huku magari yakiwafuata mara baada ya kuyanasua kwenye tope. 8 
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Bi.Esterina Kilasi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili wilayani Wanging’ombe leo, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi. 9 
“Kweli Bibi ana Huruma” Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Bibi Geremana Mrwiro mwanakijiji ambaye alileta jembe ili litumike kwa kusaidia kunasua magari yaliyokuwa yamekwama kwenye tope 10
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kijiji cha Usuka kilipo kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima wilayani Wanging’ombe ambapo Katibu mkuu wa CCM alitembelea vijana walioamua kujiunga pamoja na kuendesha kilimo . 12 
Baadhi ya vijana hao wakinyanyua kadi zao juu ili kula kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana leo. 14 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi kijana Said Mkweta.
 15 
Utulivu wa kula kiapo. 16 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi kuhuso moja ya Power Tiller itakayotumiwa na vijana hao kulimia shamba lao ili kuwahi mvua zinazonyesha. IMG_2518
Gari lililokuwa likitumiwa na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa likinasuliwa kwenye tope mara baada ya kuteleza na kuingia kandokando ya mtari IMG_2522
Juhudi za kunasua zikiendelea. 22 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipata kulia Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakitoka nje mara baada ya katibu mkuu huyo kuzindua jengo la kitegauchumi la CCM mkoa wa Njombe leo ambalo limepangishwa na Wizara ya Fedha. View detail

Monday, November 25, 2013

KINANA ASAFIRI MASAA 26 KUHAKIKISHA ANAWAFIKIA WATANZANIA WOTE

6
Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye meli ya MV.Songea cha Liuli na kuwasalimu wananchi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Kyela akitokea Wilaya ya Nyasa  mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkini wakati wa safari yake kwa kutumia ziwa Nyasa kuelekea Kyela
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu ABdulrahman Kinana akicheza ngoma ya  Mganda akishirikiana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ,Katibu Wa NEC Itikadi na  Uenezi Nape Nnauye.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akihutubia wakazi wa kijiji cha Mkini kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Kyela.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na muzaji wa samaki pamoja na mihogo ya kuchemsha kwenye bandari ya Lupingu mnamo saa saba na nusu ya usiku katikati ni Dk.Asha-Rose Migiro.
Nahodha Mkuu wa Meli ya MV Songea  Ndugu Thomas Samuel Faya akitoa maelekezo namna ya kuiongoza meli kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC Itikadi  na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka toka kwenye meli baada ya kuwasili salama kwenye bandari ya Kyela na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Siasa na Serikali.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa furaha na wakazi wa Kyela.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa Kyela waliojitokeza kuja kuwapokea.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi wa Chama na Serikali kwenye bandari ya Itungi ambayo muda si mrefu  itatengenezwa na kuanza kutumika.

View detail

Thursday, November 21, 2013

KINANA AZIDI KUJIKITA VIJIJINI (MBINGA, RUVUMA)


Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 Tawi la Amani Makolo akimkaribisha nyumbani kwake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa shina namba 9,katika tawi la Amani Makolo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Wanachama wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye  amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa Shina namba 9 Tawi la  Amani Makolo ambapo aliwapongeza kwa ushirikiano na mshikamano waliokuwa nao kiasi wameweza kuwa na wanachama hai 426.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Mtundawalo wakati akiwasili kijijini hapo tayari kwa kufanya mkutano wa hadhara.Katika Mkutano wa hadhara Katibu Mkuu wa CCM alizungumzia mipango mbali mbali ya kutatua matatizo ya wananchi na kuwaeleza wananchi CCM haiwezi kurubuniwa  kwa sababu ya kupata kura,akasisitiza wananchi wawe wa kweli kwa serikali ili haki itendeke kwa haraka.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na viongozi wengine wa CCM kulima shamba la wanawake na vijana wajasiriamali Mkwaya kata ya Kilimani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajasiriamali wa Mkwaya kata ya Kilimani ambao kwa pamoja wameamua kujishughulisha na kilimo.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakulima wa kata ya Mkwaya .
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.
Katibu wa NEC Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo Mbinga mjni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa vijijini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha  pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga  Ndugu Senyi Ngaga.
35
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbingamjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzikitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo  vya Mbinga mjini mkoa wa Ruvuma.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop