Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya,
katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii, Des 4, 2013 katika
Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa
kuhitimoisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani
ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya
kuzitatua.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi
wa msingi wa Zahanati katika kijiji cha Chamwengo Kata ya Inyala Wilaya
ya Mbeya vijijini wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo na utekelezaji
wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika ziara yake ya wilaya ya mbeya
vijijini, Katika ziara hiyo Kinana anafuatana na wajumbe wa halmashauri
kuu taifa Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na Dr. Asha
Rose Migiro Katibu wa NEC siasa na Uhusiano wa kimataifa na leo
anaendelea na ziara hiyo Jimbo la Mbeya Vijijini kabla ya kumalizia
kesho ambapo anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara
utakaofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe mjini Mbeya
Dr.
Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chamwengo kata ya
Inyala.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala wakiwa katika ujenzi wa zahanati hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigala akiliweka sawa tofali wakati
akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chamwengo kata ya
Inyala.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua tanki la
maji linalojengwa katika kijiji cha Itimu kata ya Iwindi Mbeya vjijini.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na
mjumbe mmoja wa mabalozi wakati alipokuwa akielekea kufungua shina la
CCM mjini Mbalizi.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi
kwa mmoja wa wanachama waliojiunga na chama hicho wakati alipofungua
moja ya matawi ya chama hicho mjini Mbalizi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wananchama waliojiunga katika tawi hilo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake
pamoja na viongozi wenzake wakielekea kwenye mkutano wa ndani.
0 comments:
Post a Comment