Afisa
Muuguzi msaidizi wa taasisi ya tiba ya mifupa,mishipa ya fahamu na
upasuaji wa Ubongo(MOI)katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,akitoa
ushauri kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa
wateja kuhusina na kula vyakula vyenye fuliki acid ya kutosha kama vile
mboga za majani,Matunda,Maharage na Viazi,wakati wafanyakazi hao
walipofika kutoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya
Tsh Milioni nane(8,000,000)kwa ajili ya watoto wenye ugonjwa wa kichwa
vikubwa na mgongo wazi.
Katibu
wa chama cha wazazi wa watoto wenye matatizo ya mgongo wazi na kichwa
kikubwa (ASBAHT)Bi.Hidaya Juma (kulia)akielezea jinsi mirija
inavyoingizwa kichwani wakati wa matibabu ya watoto wenye matatizo hayo
kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa
wateja wakati wafanyakazi hao walipofika kutoa msaada wa vyakula na
vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)kwa ajili
ya watoto wenye matatizo ya kichwa vikubwa na mgongo wazi.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,kitengo cha huduma kwa wateja
akifurahia jambo na mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa Ibrahim
Haji(4)anaetibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,wakati wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja walipofika kutoa
msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni
nane(8,000,000)kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na
mgongo wazi.
Wafanyakazi
wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Emmy Njau(kushoto) na
kiongozi wa kitengo hicho Geoffrey Wilfred(kulia)wakiwafariji baadhi ya
watoto wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi wanaotibiwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,walipofika hospitalini hapo kutoa
msaada wa vyakula na viti vya kutembelea vyote vyenye thamani ya Tsh
Milioni nane(8,000,000).
Muuguzi
Mkuu wa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo
wazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Bi.Haulat Daudi akielezea
umuhimu wa vifaa maalumu vinavyotumika wakati wa matibabu kwa watoto
wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi mara baada ya kukabidhiwa
na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Bi.
Harriet Lwakatare(kushoto)Jumla ya Tsh Milioni nane(8,000,000)zilitumika
katika msaada huo.
Mzazi
wa mtoto John Winfred wa kwanza toka kushoto aliekaa chini akiwaangalia
wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Bi.Leah
Ntisi na Joseph Msafiri (kulia)wanavyomweka sawa mwanae katika moja ya
viti vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Tsh Milioni
nane(8,000,000)na wafanyakazi wa kitengo hicho kwa watoto wanaotibiwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na
mgongo wazi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Kitengo cha huduma kwa wateja
wakifarijiana na wazazi wa watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili wenye kusumbuliwa na ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo
wazi,wakati wafanyakazi hao walipofika Hospitalini hapo kutoa msaada wa
vitu mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)mahususi
kwa ajili ya watoto hao.
Imeelezwa
kuwa tatizo la watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi limekuwa
kubwa zaidi tofauti na jamii inavyolichukulia tatizo hilo. Huku
ikibainika zaidi kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa kwa mwaka na ugonjwa
huo ni zaidi ya elfu huku 250 tu ndio wanafika katika taasisi ya tiba ya
mifupa, mishipa ya fahamu na upasuaji wa Ubongo (MOI)
Hayo
yamebainishwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Patrick Mvungi wakati
akipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Huduma
kwa Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia kampeni
ya pamoja na Vodacom inayoendeshwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
“Tatizo
la Ugonjwa wa kichwa kikubwa na uti wa mgongo ni kubwa sana katika nchi
yetu na linaongezeka siku hadi siku, na tunapenda kuweka wazi kuwa
tatizo hili linasababishwa na wakina mama, kuanzia wanapopata ujauzito
hadi kufikia kipindi cha miezi mitatu hapa ndipo tatizo linapotokea,
alisema, “Katika kipindi hiki mama asipokuwa anakula chakula chenye
lishe (Lishe Bora) na kwenda Kliniki kwa wakati inapelekea kupata
upungufu wa madini ya Folic acid.” Alisema Mvungi na kuongeza
“Tunahitaji
jamii ituelewe na ndipo tunapo hitaji msaada wa wadau wengine kama
Vodacom kutuwezesha kuweza kutoa elimu kwa jamii, kwa mfano hali ilivyo
sasa, watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu kwa mwaka inafikia zaidi ya elfu
nne (4000) kwa mwaka, lakini watoto tunaowapokea hapa kwa mwaka
wanafikia 250 tu. Ni jambo la kusikitisha sana. Alisema Mvungi na
kuongeza.
“Idadi
ya watoto wanaozaliwa ukilinganisha na tunaowapokea hapa kwetu ni
tofauti kabisa, wengi wanakuwa wanaamini tatizo hili linatokana na mambo
ya kishirikina na inapelekea watoto wa aina hii kuuwawa wengine
wanafichwa na wazazi wao, tunapashwa kuondokana na hali hii ili tuweze
kukabiliana na tatizo hili.” Alihitimisha Mvungi.
Akizungumzia
juu ya misaada hiyo yenye thamani ya shilingi Milioni nane Afisa Mkuu
wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Vodacom Tanzania Harriet
Lwakatare amesema kuwa kampuni yake itaendelea kuunga mkono sehemu
muhimu zinazogusa maisha ya jamii kwani wao ndio wanaowaunga mkono kila
siku.
“Tunatambua
mahitaji muhimu waliyonayo jamii ya Watanzania, hasa watoto hawa wenye
ugonjwa huu wa Vichwa vikubwa na mgongo wazi, Tumeguswa sana na maisha
ya watoto hawa na tumejisikia faraja kuwasaidia na kuwafariji,
tumefarijika kuwa sehemu ya maisha yao,” alisema Lwakatare.
Kwa
upande wake moja ya Wazazi wa watoto hao amesema kuwa amefarijika
kupokea misaada hiyo, na kuomba jamii iweze kumsaidia aweze kupata ada
ya kuendelea kumsomesha mtoto wake.
“Pamoja
na tatizo hili alilonalo mtoto wangu ameweza kujitahidi kusoma hadi
kufikia darasa la tatu lakini nimeshindwa kumuendeleza kwa sababu ya
kukosa ada ya kuendelea kumsomesha naomba kwa mtu yoyote atakae kuwa na
uwezo wa kunisaidia anisidie japo kumsomesha tu.” Alisema Mzee Joseph
Kaza, baba wa motto Selemsni Joseph (13) mwenye ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment