Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Picha mbalimbali juu ni baadhi ya wasanii chipukizi wakionesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.
Baadhi ya Wasanii chipukizi mbalimbali waliopata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.
Msanii
anaoanza kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally
Nipishe akiwaunga mkono wasanii chipukizi katika tamasha hilo.
Msanii
anaoanza kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya Ally
Nipishe (kushoto) akiwaunga mkono wasanii chipukizi katika tamasha hilo
pamoja na msanii kutoka nyumba ya vipaji THT.
Mmoja wa wasanii chipukizi akifanya vitu vyake jukwaani.
Na Mwandishi Wetu
KATIBU
Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameipongeza Asasi
ya Ukuzaji Vipaji vya Sanaa na Muziki nchini (UCA-Tanzania) kwa wasanii
chipukizi. Pongezi hizo zimetolewa jana jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo.
Bi.
Kihimbi alisema hayo alipokuwa akizinduwa tamasha la ukuzaji Vipaji vya
Sanaa na Muziki kwa vijana lililoandaliwa na asasi ya UCA-Tz kwa lengo
la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji kuonesha vipaji vyao kwa jamii
kila mwaka.
“…Nimeambiwa
kuwa asasi hii imesajiliwa kwa lengo la kuwashirikisha na kuwaunganisha
vijana wenye vipaji vya sanaa na muziki pamoja na waliokwishafanikiwa
katika kuwezesha kukuza vipaji walivyonavyo,” alisema Bi. Kihimbi
akimuwakilisha Katibu Mkuu.
“Kimsingi
hili ni jambo jema la kusaidiana na serikali katika kukuza vipaji na
kuongeza viwango vya sanaa, ili kuwawezesha wasanii wetu kukabiliana
kikamilifu katika ushindani wa soko la kimataifa,” alisema.
“…Nawashauri
vijana watumie fursa kama hii kila kila zinapopatikana katika
kufanikisha malengo yao kupitia fani za sanaa. Kama sote tunavyofahamu
kuwa sanaa ni ajira na inanafasi kubwa ya kubadili maisha ya watu na
nchi kiuchumi na kifikra ni vema watu wakaondokana na dhana potofu kuwa
sanaa si kazi ya maana na ni kwa wasiohitaji kujifunza,” alisisitiza.
Aidha
alitoa changamoto kwa badhi ya watu kuacha fikra finyu za kuichukulia
sanaa kama si kazi kama ilivyo kazi nyingine, kwani mawazo hayo
hayaitendei haki pamoja na kuzingatia umuhimi wa sanaa kwa jamii.
“…Ninapata furaha kubwa kusikia kuwa tamasha hili litakuwa likifanyika
kila mwaka. Ninakupongezeni sana kwa kubeba sura ya uzalendo unaolenga
kuikuza, kuiendeleza na kuipa hadhi fani ya sanaa na muziki,” aliongeza.
“…Ninatambua
kuwa kazi hii kubwa na nzuri mnayoifanya ni utakelezaji wa sera ya
utamaduni inayosisitiza na kusimamia maadili ya Mtanzania pamoja na
kuzingatia mafunzo na elimu katika fani zetu. Tunafahamu kuwa utamaduni
ni mali ya jamii, hivyo ni jukumu la wananchi wenyewe kuupenda,
kuuthamini na kuuendeleza utamaduni wetu kwa kutumia kazi za sanaa.”
Awali
akizungumza kabla ya uzinduzi wa tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa
UCA-Tz, Emmanuel Mushy aliishukuru Serikali kwa ushirikiano iliouonesha
kufanikisha tamasha hilo na kutoa shukrani kwa makampuni ya Zantel, Coca
Cola- Tanzania, Maezeki, LBGY Media na mtandao wa Thehabari.com
kushiriki kuwasaidia vijana wasiosikika kusikika.
Zaidi
ya wasanii 25 chipukizi walipata nafasi kwenye tamasha hilo ya kuonesha
uwezo wao kwa jamii wakiwemo baadhi ya wasanii chipukizi wanaoanza
kunufaika na kazi zao kama Menina, M Rap na Ally Nipishe.
0 comments:
Post a Comment