Mkuu
wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba (kushoto) akipitia kitabu
cha orodha ya matukio ya dawati hilo. Kulia ni msaidizi wake.
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye.
Jeshi
la Polisi Wilaya ya Nkasi kupitia dawati la Jinsia na Watoto,
linamshikilia Pius Jacob Mkazi wa Kijiji cha Chala kwa kosa la kuoa mtu
na dada yake, ambapo mdogo mtu alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano
katika Shule ya Msingi Kabwe wilayani Nkasi.
Jacob
alikamatwa na Polisi wa Dawati la Jinsia na watoto Kituo cha Nkasi
ikiwa ni wiki moja tangu amchukue kwa nguvu binti huyo wa darasa la tano
(umri miaka 12) na kuja kuishi naye kama mke na mume huku akiwa tayari
amemuoa binti mwingine wa kwanza mwenye umri wa miaka 16 ambaye pia ni
dada wa binti wa pili.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba alisema
walimfuatilia Jacob na kumkamata baada ya wao kupewa taarifa na mmoja wa
majirani wa mtuhumiwa kuwa alikuwa akiishi kinyumba na wanafunzi hao.
“…Tulikuwa
katika ziara zetu za kawaida zilizoambatana na siku 16 za kupinga
ukatili tukizunguka baadhi ya vijiji vya wilaya yetu, ndipo raia wema
walituarifu kuwepo kwa tukio hilo na kuanza kufuatilia hatimaye
kumkamata mtuhumiwa,” alisema Kisimba.
Tayari
mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desenba 10,
2013 kwa kosa la kumuoa mwanafunzi na kubaka katika Mahakama ya Wilaya
ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa kujibu mashtaka ya tuhuma zake.
Akizungumzia
tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi,
Oscar Mdenye alisema baada ya kufuatilia zaidi wamebaini hata binti (16)
aliyemuoa wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi haijulikani alitumia mbinu
gani za kumpata na kuanza kuishi naye kama mke na mume.
Aidha
ameongeza kuwa kwa mujibu wa tarifa ambazo walizipata kutoka kwa
majirani inadaiwa binti wa pili alimpata kwa kutumia nguvu na vitisho,
kwani alimfuata nyumbani kwao na kudai anakuja kuwasalimia lakini baada
ya kufika kwake alimjulisha binti huyo kuanzia sasa wewe ni mke wangu na
kuanza kuishi naye.
“…Hadi
Polisi na Ofisi ya Ustawi wa Jamii tunafikiwa na taarifa hizo inadaiwa
mtuhumiwa huyu alikuwa tayari ameishi na binti huyu wa pili kwa wiki
nzima nyumbani kwake, na majirani walijua baada ya binti wa pili (12)
kuanza kulalamika kwao kuwa alikuwa amechukuliwa kwa nguvu na
kulazimishwa kuolewa,” alisema Mdenye.
Juhudi
za kumpata mtuhumiwa kuzungumzia tuhuma zake hazikuweza kuzaa matunda
baada ya kuwa mahabusu akisubiri mwenendo wa kesi yake inayomkabili.
Hata
hivyo matukio ya ukatili yanayoripotiwa polisi kupitia Dawati la Jinsia
na Watoto Wilaya ya Nkasi yamekuwa yakipungua kutoka mwaka hadi mwaka,
kwani kwa mujibu wa takwimu za dawati hilo kwa mwaka 2012 kulikuwa na
kesi 224 za ukatili zilizoripotiwa, ilhali kwa mwaka 2013 jumla ya kesi
143 zimeripotiwa wilayani hapo.
0 comments:
Post a Comment