Welcome to our online store Portal

Template Information

Sunday, December 8, 2013

WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KTK MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU KESHO


Uhuru -1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu  kukamilika kwa maadalizi ya sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zitakazofanyika tarehe 9 Desemba  katika uwanja wa Uhuru  jijini Dar es salaam .
Uhuru -3
Vikosi vya majeshi ya Ulinzi na Usalama vya Tanzania vikiendelea na maadalizi ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru na gwaride maalum leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).
Uhuru - 2
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Zikiwa imebaki siku moja Tanzania iadhimishe miaka 52 ya Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadick ametoa wito kwa watanzania kusherehekea maadhimisho hayo kwa  kuenzi , kulinda na kudumisha mafanikio makubwa yaliyopatikana  tangu Uhuru.
Akizungumza na vyombo vya habari jana  jijini Dar es salaam Meck Sadiki amesema kuwa Tanzania katika kipindi cha miaka 52 ya Uhuru imepata mafanikio makubwa ya kiuchumi, ulinzi, usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa na kuongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na umoja na mshikamano ulioonyesha tangu kuasisiwa kwa taifa la Tanzania.
“Kipindi chote cha miaka 52 ya Uhuru  tumepata mafanikio makubwa sana na  ya kujivunia kiuchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa, tuna kila sababu ya kuendeleza mafanikio haya”

Amesema maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru kwa mwaka 2013 kitaifa yatafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete chini ya kauli mbiu isemayo “Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu, Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ya Taifa Letu”
Ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka  huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi na kupambwa na burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka bara na visiwani,Gwaride maalum la vikosi vya ulinzi na Usalama, kwaya mbalimbali, bendi za muziki, maonyesho ya ndege za kijeshi na halaiki maalum.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi  na kuwahi mapema wakati wa maadhimisho hayo   na kubainisha kuwa kutokana na maadalizi mazuri yaliyofanyika milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:30 Asubuhi.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop