Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilayani Ikungi, Olivary
Kamilly akitoa taarifa yake wakati wa makabidhiano ya majukumu kati ya
kamati iliyomaliza muda wake na ile inayotarajiwa kuanza kazi Januari
mwakani.Kush oto ni diwani (CCM) kata ya Ikungi, Haji Mukhandi na
katikati ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo aliyemaliza muda wake
Naftal Gukwi.
Diwani
wa kata ya Ikungi wilaya ya Ikungi,Haji Mukhandi akitoa nasaha zake
wakati wa hafla ya makabidhiano baina ya kamati ya shule ya msingi
Ikungi mchanganyiko iliyofanyika shuleni hapo.
Mwenyekiti
wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko aliyemaliza muda wake,
Naftali Gukwi (kulia) akikabidhi hati ya makabidhiano Mwenyekiti
mteule, mwalimu mstaafu,Rashid Msaru.
Baadhi
ya wajumbe wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko na baadhi
ya walimu,wakifuatilia ajenda za mkutano wa dharura wa kamati ya shule
hiyo.
(Picha na Nathaniel Limu).
Mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko Wilaya ya Ikungi, Olivery
Kamilly amewataka wazazi na walezi kufuatilia kwa karibu maendeleo ya
watoto wao shuleni ili pamoja na mambo mengine kuthibiti utoro
unaochangia kushusha kiwango cha taaluma.
Kamilly
ametoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati akizungumza muda mfupi
baada ya kamati ya zamani kukabidhi majukumu kwa kamati teule
inayotarajiwa kuanza kazi Januari mwakani.
Amesema utoro wowote uwe wa reja reja au ule sugu unachangia mwanafunzi asiwe na mtiririko mzuri wa masomo.
Akifafanua
zaidi amesema,“Matunda ya utoro ni mwanafunzi kufanya vibaya kwenye
mitihani yao. Ili hili lisitokee tena ushirikiano baina ya wazazi na
walezi, walimu na kamati ya shule uimarishwe ili kudhibiti utoro kwa
wanafunzi”.
Aidha,
mwalimu Kamilly alitaja baadhi ya majukumu ya kamati ya shule kuwa ni
pamoja na kusimamia uandikishaji wa elimu ya awali na wa darasa la
kwanza.
Alitaja
majukumu mengine kuwa ni kuhakikisha shule inajitosheleza kwa miundo
mbinu bora kwa vile majengo, samani na vifaa vya kujifunzia na
kujifundishia na kubuni na kutafuta vyanzo vya mapato kwa ajili ya
kugharamia shughuli zilizopo kwenye mpango wa maendeleo ya shule.
Kwa
mujibu wa mwalimu Kamilly, shule hiyo iliyoanzishwa 1944, inakabiliwa
na changamoto mbali mbali ikiwemo ya ukosefu wa ushirikiano wa baadhi ya
wazazi na uongozi wa shule na hasa wazazi wenye watoto wenye ulemavu.
“Pia
shule haina mtandao wa mabomba ya maji shuleni na hii inasababisha
watoto wenye ulemavu wa uoni na ngazi kufuata maji kwa matumizi yao
umbali mrefu ambao ni hatari kwa maisha yao”,amesema mwalimu Kamily.
Kwa
upande wake Mwenyekiti Mteule wa kamati ya shule hiyo, Rashid Msaru
aliahidi kuwa kamati yake itakuwa daraja zuri kati ya shule na serikali
za vijiji, na kati ya walimu na wazazi na walezi.
Aidha, Msaru aliahidi kuwa kamati yake itakuwa ni ya maendeleo ya shule tu na wala siyo ya kudhibiti walimu.
0 comments:
Post a Comment