Watu wanne wakazi wa Kijiji cha Nyankumbu mkoani Geita, wameuawa
kikatili kwa kuchomwa moto na mwingine akifia kwenye dimbwi la maji
kijijini hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa wa
Polisi mkoani hapa, Leonard Paul alisema kuwa tukio hilo la kikatili
lilitokea usiku wa juzi.
Paul alisema saa sita usiku watu wanaokadiriwa
watano walikwenda nyumbani kwa Mzee Barabara Luhemeja kwa lengo la
kupora fedha .
“Watu hao walikwenda kwenye nyumba ya Luhemeja na
kumkuta mtoto wake waliyemtaka kuwaonyesha mahali alipo baba yake,”
alisema Kamanda Paul.
Alisema kuwa wakati wakiendelea kumhoji mtoto huyo
awaonyeshe baba yake, ghafla alitokea ambapo watu hao walimweka chini
ya ulinzi kabla ya kupora Sh60,000 ambazo ni rambirambi ya kufiwa na
mjukuu wake.
Paul alisema kuwa baada kupora fedha hizo,
walikimbia, ambapo mzee huyo alitoa kwa sungusungu walioanza msako wa
watu haona kubahatika kumkamata mmoja aliyewataja wenzake.
Baada ya watuhumiwa wote kukamatwa, wananchi waliwafunga kamba na kuwachoma moto.
Akizungumza kwa huzuni, mama mmoja ambaye jina
lake halikupatikana, ambaye pia miongoni wa waliouawa ni watoto wake,
alisema: “Ndiyo kwanza napata taarifa kwamba watoto wangu walikuwa
wezi,” Nyambona Malwa alisema kuwa hana taarifa.
Aidha Kamanda alisema kuwa watu waliouawa katika
tukio hilo majina yao hayajafahamika, kwani walikuwa wageni kwenye
kijiji hicho.
Kamanda Paul ameonya tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi, kwani jeshi lake halitasita kuwachukulia hatua kali.
“Mpaka sasa tunawashikilia watu watatu kwa tuhuma
za mauaji ya watu hayo na uchunguzi wa kuwabaini wengine unaendelea,”
alisema Kamanda Paul.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Said Magalula naye ameonya
tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi, akisema kamwe
haivumiliki na kuwataka kuacha vitendo hivyo mara moja.
“Mwizi akikamatwa, asiuawe, wananchi watoe taarifa kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe kama kupekwa kortini.”
“Mwizi akikamatwa, asiuawe, wananchi watoe taarifa kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe kama kupekwa kortini.”
0 comments:
Post a Comment