Watu saba wamefariki dunia katika matukio tofauti wakati wa
Sikukuu ya Krismasi mkoani Morogoro, akiwemo mtoto wa mwaka mmoja kuuawa
na watu wasiofahamika kisha kukatwa sehemu zake za siri na mwili wake
kutupwa pembezoni mwa Mto Morogoro.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro
Faustine Shilogile alimtaja mtoto aliyefariki kuwa ni James Stephen
(1), mkazi wa Nanenane Manispaa ya Morogoro na kwamba tukio hilo
lilitokea Desemba 25 mwaka huu saa moja asubuhi.
Katika tukio la pili, mtoto Veronica Chigunda (6)
mkazi wa Mashambani Likwambe, Wilaya Ulanga alifariki dunia wakati
akipelekwa Hospitali ya Lugala baada ya kuungua moto wakati amelala
kwenye nyumba anayoishi.
Kamanda Shilogile alisema kuwa tukio hilo
lilisababisha majeraha kwa watu wawili, akiwemo mama wa marehemu Paula
Fimbo (24) na Matiasi Mahumba (1) na wote wamelazwa katika hospitali
hiyo.
Shilogile alisema tukio la nne, mfugaji wa jamii
ya kimasai Mela Kipara (25) mkazi wa Makole wilayani Mvomero, alifariki
dunia baada ya kukatwa na mapanga na mfugaji mwenzie wakati wakitoka
kunywa pombe za kienyeji.
Aidha, Mganga Machaku (35) mkazi wa Mdudu, Kilosa
alikutwa ndani ya nyumba yake amekufa na mwili wake ukiwa umeharibika
vibaya huku chanzo cha kifo hicho kikiwa ni kunywa pombe za kienyeji
kupita kiasi.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu Dar es Salaam, limejipanga kuongeza ulinzi katika kuelekea
mkesha wa Mwaka Mpya.
0 comments:
Post a Comment