Welcome to our online store Portal

Template Information

New Products
Showing posts with label Bunge la katiba. Show all posts
Showing posts with label Bunge la katiba. Show all posts

Monday, April 7, 2014

SAHIHI ZA HATI YA MUUNGANO ZAZUA UTATA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta kukiri kuchezewa kwa saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Msekwa amesema, ‘mzungumzaji huyo ana lake jambo’.

Sitta akizungumza na mwandishi wetu  juzi mjini Dodoma alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.
Alifafanua kuwa saini ya Nyerere imeongezwa herufi ‘us’ kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno ‘Msekwa’ kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.
Msekwa akizungumza na mwandishi weu jana alisema: “Saini iliyo katika hati original (halisi) ni ya kwangu mimi, lakini huyo anayesema zimechezewa muulizeni atakuwa na lake jambo. Kama kompyuta imekosea ni leo kwa kuwa kipindi hicho kompyuta hazikuwapo.”
Aliongeza: “Ana lengo gani la kutilia shaka, ana lengo gani la kusema imechakachuliwa, kinachotakiwa ni hati original ambayo iko ofisi ya Katibu wa Bunge itolewe, kwanini tuendelee kuandikia mate wakati wino upo?”

Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Taarifa kwa Wananchi Umma (TCIB), Hebron Mwakagenda alisema yote hayo yanatokea ni kuvuruga hoja iliyopo mezani.
Alisema kitendo cha kupoteza muda kuzungumzia suala la kuchezewa kwa saini halitakiwi kwani kama maudhui yake hayakuchezewa basi hoja ya muundo wa Muungano uamuliwe na wananchi wenyewe.
“Tusianze kupoteza muda kwa mambo ambayo hayapo cha msingi wananchi wenyewe waulizwe wanaupenda Muungano au la lakini tusianze kumtafuta mchawi kuwa saini zimechezewa wananchi waamue wenyewe kuhusu Muungano,” alisema Mwakagenda.

Utata huo ulianza wiki hii baada ya kamati za Bunge Maalumu la Katiba kuanza vikao vyake vya kujadili sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wake.
Hali hiyo ilitokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa Muungano.
Aprili 2 mwaka huu, Kamati namba 2 ilimwalika, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo, lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali. Msekwa aliitwa kutokana na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha, alithibitisha kutokea utata huo na kwamba walilazimika kumuita Msekwa ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa na Msekwa alisema saini zilizopo katika hati hiyo ni ya kwake.
Nahodha alisema kwa maelezo ya Msekwa, inaonekana hati ya Muungano ipo Umoja wa Mataifa (UN), kwani kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa na kiti chake UN na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hali kadhalika.
Aliongeza kuwa baada ya UN kuomba uthibitisho wa Muungano, ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.
Kwa upande wake Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad alisema hati hiyo ipo Dar es Salaam na ni moja tu, hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.
View detail

Friday, March 28, 2014

TUHUMA NZITO DHIDI YA WAZIRI MKUU BUNGENI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hali ya hewa jana ilichafuka kwenye Bunge la Katiba baada ya mjumbe Ezekiel Wenje kuwatuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziri kuwa waliwahonga baadhi ya wajumbe wa kundi la 201.
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo, huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.

Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana (Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani “walilia” sana kuwa Bunge la Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:“…Sasa kuna wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki.”
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa Maghembe alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
“Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi ya kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa taratibu za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia chakula, hakuna anayeweza kupewa rushwa.
“Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi,” alisema Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Makamu mwenyekiti pia alifanya jitihada za kuwataka wajumbe kuwa wavumilivu, huku akitoa nafasi kwa Dk. Kawambwa kujieleza akisisitiza kwamba ni tuhuma nzito. 
Kawambwa alisema: “Ni kweli nilikutana nao; ni wajumbe ambao wanatoka kwenye taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu, lakini mbona wameshafanya mikutano yao mingine mingi ambayo mimi hawakuniita. Kama mtu akiwa hana hoja bora akae chini.”
Makamu Mwenyekiti alimtaka Wenje aombe radhi kutokana na kauli yake, lakini katika hali ya kushangaza mjumbe huyo alisisitiza kwamba Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamekiri.
“Maghembe amekiri aliwaita wafugaji na wavuvi ndiyo waliokula chakula cha rushwa, pia wapo wengine walienda kwa Waziri Gaudensia Kabaka, kuna ushahidi mama mmoja siwezi kumtaja jina hapa alikwenda huko akafukuzwa, nitakupa jina lake mwenyekiti baadaye. Aliambiwa kwamba anatoa siri… hoja iliyojadiliwa huko ilikuwa ni kwamba msimamo ni wa serikali mbili… rushwa ya chakula, maji na bahasha walipewa,” alisema Wenje na kusababisha kulipuka kwa kelele zaidi.
Wenje aliongeza kuwa kuna wajumbe wengine walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00 usiku.
Alisema wengine walikwenda kwa Gaudensia Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha.
Baada ya Wenje kukaa, baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 walichachamaa wakitaka kutetea hadhi yao, akiwamo mjumbe kutoka kundi la wafugaji, Esther Juma aliyesema hawatendewi haki kama kundi kusema kwamba walihongwa.
Alisema yeye ana ng’ombe 3,000 na asingeweza kwenda kupokea rushwa ya chakula na kumtaka mbunge huyo kuwaomba radhi la sivyo asingetoka mlangoni.
Wakati mjadala huo ukiendelea, mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta aliyekuwa ametoka kwa udhuru, alirejea kimya kimya, na kumtaka Wenje kueleza iwapo anadhani kauli yake haikuwaudhi baadhi ya wajumbe.
Wenje alikiri kuwa ni kweli baadhi ya wajumbe wameudhika kutokana na ukweli aliosema dhidi yao na kuwaomba radhi kwa ukweli huo.
Kauli hiyo ilimfanya Sitta kutangaza kuwa anapeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge na uamuzi utakaotolewa atautangaza bungeni.
View detail

Thursday, March 27, 2014

HALI HALISI BUNGE LA KATIBA

http://azizicompdoc.blogspot.com/  “Uvumilivu una mwisho wake, ukifika wakati huo tutawaambia Watanzania nini kinachoendelea na sisi tunakusudia kufanya kitu gani.”PICHA|MAKTABA
Kuna njama. Maneno haya mawili ndiyo yametumiwa na pande mbili zinazopingana ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, kuelezea hali iliyojitokeza jana wakati wa kikao cha Bunge hilo kuhusu mvutano wa mabadiliko ya kanuni.
Njama zinazoelezwa na pande hizo ni za kuvuruga mchakato wa Katiba Mpya, zikirejea yaliyotokea jana jioni ikiwamo zomeazomea hali iliyomlazimu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuliahirisha Bunge hadi leo jioni.
Baada ya kuahirisha Bunge hilo, Sitta alikutana na waandishi wa habari na kusema kwamba kuna njama za baadhi ya wanasiasa kutumia vurugu kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba, badala ya kujenga hoja.
Bila kuwataja wanasiasa hao, Sitta alisema ikiwa hawataki kuendelea na mchakato huo, basi waondoke na kuwaacha wenye nia njema.
“Wanasiasa hawa wamedhamiria kuvuruga mchakato wa Katiba, tuhuma ambazo tumetuhumiwa leo na Lissu (Tundu) ni uongo na uzushi, mimi sihusiki na kupeleka marekebisho ya kanuni kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge,” alisema Sitta.
Sitta alikuwa anajibu mchango wa mjumbe wa Bunge, Tundu Lissu alioutoa mapema kwenye kikao cha jioni, akipinga kilichoelezwa ni njama za kutaka kubadili kanuni kinyemela ili kumsaidia mwenyekiti kulidhibiti Bunge.
Sitta alisema kwa kuzingatia kanuni ya 59 (1), Kamati ya Uongozi ina mamlaka ya kupeleka marekebisho ya kanuni ili kuliwezesha Bunge kufanya kazi vizuri.
Alisema hoja kwamba haiwezekani kufanyika mabadiliko hata kabla ya kuanza kutumika kanuni, siyo ya msingi kwani kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira yake.
“Kamati ya Uongozi ndiyo ilipeleka waraka wa mabadiliko ya kanuni kwa Kamati ya Kanuni na Haki kwa kuzingatia kanuni, lakini hata kabla ya kujadiliwa na kamati husika inaonekana kuna wajumbe ndiyo wameichukua na kuifikisha bungeni,” alisema Sitta.
Alisema kwa kiasi kikubwa marekebisho ambayo yangesomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pandu Ameir Kificho, yalilenga kutoa ufumbuzi wa kanuni ya 37 na 38 juu ya upigaji kura ama uwe wa wazi au siri.
Sitta alisema pamoja na hilo, kulikuwa na marekebisho ya msingi kama kuweka utaratibu mzuri wa majadiliano katika kamati pia kuweka utaratibu wa vikao vya Bunge kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.
“Mengi ambayo alikuwa anayasema Lissu kama ni takataka hayakuwapo katika taarifa ya Kificho,” alisema Sitta.

Kauli ya Lissu
Lissu katika mchango wake alibainisha kile alichoeleza kama ‘njama’ za kuchakachua kanuni, akihoji inawezekanaje kasoro zikaanza kuonekana wakati kanuni hazijaanza kutumika.
Alisema kanuni zilipitishwa mapema mwezi huu na kiporo pekee kilikuwa ni ile ya 37 na 38 kuhusu upigaji kura.
“Tumeletewa jedwali la marekebisho ambalo linaonyesha kuna marekebisho katika kanuni ya 14 (1), 32, 33, 35 na zile za 37 na 38 pamoja na 58(1) (d) zingine ni 63 (1) na 64 na kufutwa kwa kanuni ya 85, jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni zetu,” alisema Lissu.
Mbunge huyo wa Singida Mashariki, alisema utaratibu wa kurekebisha kanuni umeelezwa katika kifungu cha 87 (2) kwamba, mjumbe akiona kuna hitaji la kurekebisha kanuni awasilishe pendekezo kwa mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Kanuni na iwapo Mwenyekiti akiona inafaa atawasilisha mapendekezo hayo bungeni.
“Kanuni hazina hata wiki tatu, hazijaanza kutumika tayari mmeanza kuzichakachua hivi, kasoro mmezipataje wakati bado hazijaanza kutumika,” alihoji.
Huku akionyesha marekebisho hayo, Lissu alisema: “Hizi ni takataka ambazo hatutakubali ziingizwe ndani ya mabadiliko.” Alisema Kamati ya Uongozi haina mamlaka yoyote juu ya kanuni za Bunge.
Lissu kushtakiwa
Sitta alisema kutokana na lugha alizotumia Lissu juu yake, anakusudia kumfikisha kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge. Alisema atatoa utetezi na wale ambao wanamtuhumu wataeleza ili ukweli ujulikane.
Alisema vurugu za jana jioni, zilipangwa hata kabla ya kuanza Bunge hilo, kwani hata wajumbe wanaotokana na Ukawa walisusia kutoa maoni katika Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge.
“Wajumbe wao hata kwenye kamati walikuwa hawazungumzi na wakati wanatoka walisikika wakisema wataendelea na mkakati wao wa kufanya vurugu,” alisema Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dalili za kuvunjika kikao hicho zilionekana mapema baada ya wajumbe kuingia ukumbi kwani baadhi walikuwa kwenye makundi yaliyoashiria kujipanga kwa jambo lililokuwa mbele yao.
Kwa muda kidogo ukimya ulitawala bungeni baada ya Sitta kuzungumza, kisha ilisikika sauti ikiomba mwongozo.
Mwenyekiti alitoa nafasi kwa Lissu akitimiza ahadi yake aliyokuwa ameitoa asubuhi kabla ya kuahirisha Bunge hilo.
Mapema jana asubuhi, Sitta alikuwa ameahidi kuwa angetoa nafasi kwa miongozo hata kama ingekuwa 20 au 30 ili kila mtu aweze kupata kile alichokuwa akikihitaji.
Baada ya Lissu kueleza tuhuma zake, zomea zomea ilianza bungeni kiasi cha kuvuruga na kuondoa utulivu.
Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary baada ya kuruhusiwa alisema Bunge linaendeshwa na kanuni “haiwezekani huko aliko aandike mambo yake na kuyapeleka kwenye kamati halafu yaletwe bungeni, jambo hili haliwezi kukubalika.”
Alisema Bunge hilo ni lenye hadhi na heshima kubwa lakini kanuni kukiukwa kwa kanuni na sheria husika kunapunguza hadhi yake.
Kauli za wajumbe hao ziliungwa mkono na mjumbe mwenzao Ismail Jussa ambaye alisema waliopendekeza mabadiliko ya kanuni walikaa mafichoni kutekeleza azma hayo.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, akizungumza huku akikatishwa na makofi yaliyochanganyika na zomeazomea na yeye akielekeza maneno yake kwa kelele hizo alisikika akisema, “sijazoea kuzomewa” na wakati mwingine akisema “sijazoea kupigiwa makofi.”
Baada ya utulivu kukosekana, Sitta aliahirisha Bunge hilo ili kwanza wajadiliane kabla ya kuendelea.

Wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wamesema wataendelea kupambana ndani ya Bunge Maalumu hadi ipatikane Katiba nzuri na watakuwa wa mwisho kujitoa katika mchakato huo.
Pia wamebainisha kuwa kukimbia au kujitoa katika mjadala huo ni sawa na kuwaachia CCM walio wengi kwenye Bunge Maalumu watunge Katiba wanayoitaka wenyewe na hivyo kuzima mawazo ya wananchi.
Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe alitoa msimamo huo jana katika mkutano na waandishi wa habari huku akiweka tahadhari kuwa “Uvumilivu una mwisho wake, ukifika wakati huo tutawaambia Watanzania nini kinachoendelea na sisi tunakusudia kufanya kitu gani.”
Imeandikwa na Mussa Juma, Habel Chidawali na Editha Majura
Mbowe ambaye ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuna dalili zinavyoonyesha kuwa CCM hakina nia njema ya kuwafanya wananchi wapate Katiba nzuri.
“Hakuna mwendawazimu ambaye anaweza kufanikiwa kutugombanisha na kutusambaratisha, lazima katika jambo hili tutashinda na matakwa ya wananchi yatachukua nafasi ndani ya Katiba.”
Kwa upande wake James Mbatia alisema Ukawa haiwezi kwenda kinyume na wala haitakuwa tayari kuwasaliti wananchi katika yale ambayo waliyapendekeza kwenye rasimu.
Hotuba za JK, Warioba kutojadiliwa
Matarajio ya wajumbe wa Bunge Maalumu kujadili hotuba ya Rais Jakaya Kikwete na ile ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba yameyeyuka.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alisema amechukua uamuzi huo baada ya majadiliano ya kina na kuonekana ni kama kutanguliza mjadala wa Rasimu ya Katiba kabla ya wakati wake.
“Kumbukeni waheshimiwa Rasimu ya Katiba tutaijadili kwa mpangilio wa sura mbili kama haitafanyika marekebisho ya kanuni hivyo, tukijadili hotuba hizi, wabunge watajadili mahala popote panapowahusu na hivyo itaharibu kabisa utaratibu wa kanuni,” alisema Sitta.
Awali, ilipangwa hotuba hizo kujadiliwa hasa kutokana na hoja mbalimbali za wajumbe kutaka kujadiliwa hutuba hiyo.
Miongoni mwa wajumbe walioomba kujadiliwa kwa hotuba hizo ni Julius Mtatiro ambaye pia aliomba kurejeshwa kwa Jaji Warioba kutoa ufafanuzi kuhusu masuala yaliyoibuliwa na Rais Kikwete.

Mjumbe mwingine Tundu Lissu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa alikuwa anakusudia kumjibu neno kwa neno Rais Kikwete katika kila hoja kwani hotuba yake ilikuwa na upungufu.
View detail

Tuesday, March 18, 2014

SERIKALI TATU KUONGOZA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Jaji Sinde Warioba leo aweka wazi kwanini tume yake ilipendekeza serikali tatu kwa nia ya kudumisha muungano pamoja na changamoto kutokosekana ila kuna uwezo mkubwa wa kuondoa kero nyingi za muungano na kudumisha muungano wetu, suala la ukubwa na uzito wa serikali hizo amesema ni suala la kawaida na sio zito kama linavyofikiriwa na wengi ktk nchi, uthubutu lazima uwepo tukitaka kuishi bila migongano ktk muungano wetu.
Katika kuielezea Zanzibar kuhusu changamoto za muungano amesema kiuhalisia huwezi kuikataza leo znz isiitwe nchi na wakati katiba ya nchi hiyo inatambua kama nzn ni nchi kamili ktk muungano wa nchi mbili yaani Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa Tanganyika. Mamlaka ya viongozi wa nchi ya znz yalionekana kuchukuliwa na Rais wa muungano na baadae kurudishwa kupitia katiba mpya ya Zanzibar, kitu ambacho kwa sasa ni kigumu kutokana na sheria zinazotungwa na bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuonekana hazitatumika znz mpaka baraza la wawakilishi znz litakapozipitia na kuzipitisha sheria hizo.

Mgawanyo wa mapato ya muungano umekua mgumu na kusababisha mapato ya muungano kutumika zaidi ktk upande mmoja wa muungano ambako ni Tanzania bara. Akaunti ya pamoja ni miongozi mwa mambo ya makubaliano ktk muungano lakini limekua gumu mpaka sasa kufanyiwa kazi, Mamlaka ya waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano ni mpaka zanzibar, lakini haonekani waziri mkuu kukagua miradi ya maendeleo zanzibar, halikadhalika kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania haonekani kufanya hivyo kwa zanzibar.
Suala la Tanganyika kujificha ktk koti la muungano limedhihirishwa dhahir leo bungeni na Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Sinde Warioba na kuwaasa wajumbe wa bunge hilo kua makini na maamuzi yao ili kufikia mafanikio mazuri ya kudumisha muungano wetu na kusema ye na wajumbe wenzake wametoa pendekeze la kua na serikali tatu badala ya mbili za sasa kama inavyotambua katiba yetu.

Rasimu hiyo imeonyesha kuvuta hisia za wajumbe wengi wa bunge maalum na kutoa ahadi za kufanya vizuri zaidi ktk maamuzi yao kama alivyotoa shukrani zake makamu mwenyekiti wa bunge maalum Mh Samia Suluhu. Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki Afrika

View detail

Monday, March 17, 2014

BUNGE LASITISHWA GHAFLA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hali hiyo imetokea ghafla saa 11 jioni baada ya mwenyekiti wa mabadiliko ya katiba Jaji Warioba kuingia ktk bunge na wabunge wa bunge maalum  kuamua kupiga meza kama kumpongeza mwenyekiti kwa kuja na kutoacha kupiga meza kwa zaidi ya robo saa, na walipotakiwa kuacha wakawa wanaendelea mpaka pale mwenyekiti wa kudumu Mh Samwel Sitta alipoamua kuliahirisha bunge hilo mpaka itakapotangazwa tena. Je watanzania ni mabadiliko ya kidemokrasia au utovu wa nidhamu na utumiaji mbovu wa rasilimali za watanzania? jibu na maamuzi tunayo sisi wenyewe na kuamua watu hawa kuwarudisha tena bungeni msimu ujao au kuwaondoa wakajifunze tabia. Mali na muda wa watanzania unapotea bila sababu kwa umbumbumbu wa watu wachache, kuna haja ya mabadiliko nchini kwetu View detail

Thursday, March 6, 2014

WAJUA KILICHOSABABISHA BUNGE MAALUM KUAHIRISHWA?


Mjumbe wa bunge la Katiba,pia ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho cha bunge.

Endelea kutufuatilia uendelee kugabarika kuhusu suala hili
View detail

Wednesday, March 5, 2014

HATI YA MUUNGANO YAZUA TAFRANI BUNGE LA KATIBA

USAWA WA JINSIA NI WINGU ZITO BUNGE LA KATIBA

bunge
Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.

Suala la Jinsia katika uongozi wa Bunge Maalum la Katiba limeibua Mjadala mzito katika nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge hilo Lediana Mung’ong’o ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua suala hilo wakati wa mjadala kuhusu marekebisho ya kanuni za bunge kipengele 8(i) kinachozungumzia utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
Mung’ong’o alitaka kipengele hicho kuzingatia uhusiano wa kijinsia, ambapo kama mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume.

“Mwenyekiti hili suala la Mwenyekiti na Makamu wake hatuna budi kuangalia suala la jinsia kwamba ikiwa mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume” amesema Mung’ong’o.
Naye Mjumbe wa Bunge hilo Anna Abdalah amesema kuwa suala hilo lilikosewa Tangu awali hivyo hakuna budi makubaliano yafanyike kwa busara maana wanawake wenye sifa na uwezo wapo wengi Tanzania Bara na Zanzibar.

Akichangia katika suala hilo Mjumbe wa Bunge Hilo ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha Adam Malima amesema kuwa ili kuwepo kwa amani na Mshikamano sheria haina budi kusema wazi endapo Mwenyekiti atatoka Tanzania Bara basi Makamu wake atoke Zanzibar.
Akijibu hoja hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman amesema kuwa suala hilo liwe la marekebisho lakini si kwa kuvunja sheria hiyo.
“Sharti hilo likibadilishwa litakuwa ni kituko na tutakuwa tunarekebisha sheria ambazo hazikutungwa na Bunge Maalum la Katiba hivyo ni busara kufanya makubaliano ili kufikia muafaka wa jambo hilo” amesemaOthman Masoud Othman.
View detail

Monday, February 24, 2014

SAKATA LA MJUMBE FEKI BUNGE LA KATIBA LACHUKUA SURA MPYA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Ofisi ya Bunge la Katiba, imemwandikia barua mwajiri wa Amina Mweta, ambaye alisaini posho ya Bunge hilo ili akatwe posho aliyoichukua katika mshahara wake.
Akizungumza na Blog hii jana katika Ofisi za Bunge mjini hapa, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Thomas Kashililah, alisema Bunge limechukua hatua hiyo baada ya Mweta kuwajibu kuwa fedha walizompatia alikuwa ameshazitumia.
“Yeye (Amina Mweta), ni mwajiriwa wa Halmashauri ya Mwanga, tulichokifanya ni kumwandikia barua mwajiri wake ili akatwe katika mshahara wake,” alisema na kuongeza: “Atajua mwenyewe kama atalipa kwa kukatwa kidogo kidogo ama yote, lakini lazima ailipe posho hiyo aliyoichukua, kwa sababu alichukua na kuweka sahihi.”
Blog hii lilikuwa la kwanza kuripoti baada ya kutokea utata huo wa majina mawili ya wajumbe kufanana huku ikielezwa kuwa wote walikuwa wamesaini fomu za fedha za posho ya kujikimu ya Sh80,000 kwa siku kwa muda wa siku 13 unaomalizika Februari 28 mwaka huu ikiwa na maana kwamba kila mmoja alilipwa Sh1,040,000.
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, awali, alipoulizwa kuhusu utata huo alisema mjumbe halali ni yule aliyetoka Songea.
Hata hivyo, alisema kinachowashangaza ni kwamba yule mwenzake wa Mwanga alipotakiwa kurudisha fedha alizopewa kimakosa alisema ameshatumia sehemu kubwa na kubakiza Sh50,000 tu.
Akizungumza na Blog hii, Mweta kutoka Mwanga alisema alipigiwa simu na Ofisi ya Bunge Maalumu la Katiba na kupongezwa kwa kuteuliwa na Rais kuwa mjumbe. “Mimi ni personal secretary (katibu muhtasi) wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na nilipigiwa simu na Ofisi ya Bunge wiki iliyopita nikipongezwa kwa uteuzi huo,” alisema.
Alisema alipofika na kujisajili baada ya kutoa kitambulisho chenye jina lake, alipewa kitambulisho na kisha kupewa malipo yake ya posho.
Naye Mweta kutoka Songea alisema alipigiwa simu na Katibu Mkuu wa COTWU kwamba aliteuliwa na Rais kuwa mjumbe na kutakiwa kuripoti bungeni.
Tayari Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limeeleza kusikitishwa na utata wa watu hao wawili wenye majina yanayofanana kuwasili katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma kwa nafasi ya ujumbe wa Bunge hilo, huku likisema halimfahamu Amina Mweta wa Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya mapema alikaririwa na Blog hii akisema kuwa mazingira ya tukio hilo yamewatisha, hivyo kulazimika kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ili kumthibitisha mjumbe wao halali.
View detail

SUALA LA POSHO BUNGE LA KATIBA LACHUKUA SURA MPYA

 ONGEZEKO LA POSHO LIMEKWAMA;Binafsi namshukuru sana mungu!Taarifa rasmi ambazo nimezithibitisha kutoka katika vyanzo muhimu na vya kuaminika vya bunge, serikali na wadau wengine zinathibitisha kuwa ishu ya ongezeko la posho imekwama na KUFA KIFO CHA MENDE.Hii ina maanisha kwamba wajumbe wa bunge maalum la katiba watalipwa shs 300,000 tu kwa siku kama ilivyokuwa hapo awali.Narudia tena kwamba jambo hili limekwama na halitakuwepo.Leo saa 2.00 asubuhi nilipanga kuanzisha zoezi la kukusanya SAINI za wajumbe wote wanaopinga ongezeko la posho, ni kazi ambayo ingenigharimu siku tatu kuisimamia.Natangaza rasmi kusitisha zoezi la kukusanya saini kwa sababu ULAFI huu wa posho uliopendekezwa na baadhi ya wabunge wa CCM umekatishwa kwa maslahi ya umma.Nawaomba watanzania wote kuelekeza mijadala yetu kwenye rasimu ya katiba na tuondoke kwenye suala la posho ambalo limefika mwisho.Nataraji leo, Mwenyekiti wa muda wa bunge maalum atathibitisha kuwa hakuna ongezeko la posho.Nawashukuru sana Wabunge na Wawakilishi wa Chama cha Wananchi CUF ambao walinitia moyo na kuchangia gharama za mabango maalum yenye picha za kuonesha mateso ya kina mama wanapojifungua, na lile la kuonesha watoto wa shule walivyokaa juu ya mavumbi(ambayo yangetumika katika zoezi hili).Namshukuru sana Prof. Ibrahim Lipumba na Zitto Kabwe kwa kuniunga mkono katikati ya jambo hili. Nawashukuru baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba ambao walikuwa tayari kusaini PETITION leo hii na waliopinga ULAFI huu.Mungu ibariki Tanzania.
Taarifa rasmi ambazo nimezithibitisha kutoka katika vyanzo muhimu na vya kuaminika vya bunge, serikali na wadau wengine zinathibitisha kuwa ishu ya ongezeko la posho imekwama na KUFA KIFO CHA MENDE.
Hii ina maanisha kwamba wajumbe wa bunge maalum la katiba watalipwa shs 300,000 tu kwa siku kama ilivyokuwa hapo awali.
Narudia tena kwamba jambo hili limekwama na halitakuwepo.

Leo saa 2.00 asubuhi nilipanga kuanzisha zoezi la kukusanya SAINI za wajumbe wote wanaopinga ongezeko la posho, ni kazi ambayo ingenigharimu siku tatu kuisimamia.
Natangaza rasmi kusitisha zoezi la kukusanya saini kwa sababu ULAFI huu wa posho uliopendekezwa na baadhi ya wabunge wa CCM umekatishwa kwa maslahi ya umma.
Nawaomba watanzania wote kuelekeza mijadala yetu kwenye rasimu ya katiba na tuondoke kwenye suala la posho ambalo limefika mwisho.

Nataraji leo, Mwenyekiti wa muda wa bunge maalum atathibitisha kuwa hakuna ongezeko la posho.
Nawashukuru sana Wabunge na Wawakilishi wa Chama cha Wananchi CUF ambao walinitia moyo na kuchangia gharama za mabango maalum yenye picha za kuonesha mateso ya kina mama wanapojifungua, na lile la kuonesha watoto wa shule walivyokaa juu ya mavumbi(ambayo yangetumika katika zoezi hili).
Namshukuru sana Prof. Ibrahim Lipumba na Zitto Kabwe kwa kuniunga mkono katikati ya jambo hili. Nawashukuru baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba ambao walikuwa tayari kusaini PETITION leo hii na waliopinga ULAFI huu.
Mungu ibariki Tanzania.



View detail

Thursday, February 20, 2014

MTU NA MKEWE WAZUA BALAA BUNGE LA KATIBA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia chama hicho kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya Muungano.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD - Zanzibar, Khamis Haji Mussa katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari mjini hapa juzi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk Emmanuel Makaidi amewasilisha majina mawili, la kwake na la mkewe, Modesta Ponera kwa ajili ya uteuzi.
Alisema NLD - Zanzibar kilianza kufuatilia taratibu za uwasilishaji wa barua tangu Desemba 27, mwaka jana kwa kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ baada ya kupokea maelekezo ya Ikulu ya Tanzania kwamba majina ya Zanzibar yatafanyiwa kazi visiwani na ya Bara yangepelekwa Ikulu Dar es Salaam.
Alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vilitakiwa kila kimoja kutoa mtu mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar ili kuwa na sura ya kitaifa, lakini Dk Makaidi alikiuka utaratibu huo.
 
Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Makaidi alikiri kuwa Ponela ni mke wake, lakini akasema ni mwanachama wa NLD, hivyo ana haki ya kuteuliwa.
Alisema alipeleka majina manne Ikulu na kwamba upande wa Zanzibar ulitakiwa kufanya hivyo kupitia Ikulu ya Zanzibar... “Walifanya uzembe, hawakupeleka majina ya wanachama wa NLD, matokeo yake nikapeleka majina manne, tukapata uwakilishi.”
 Alisema mkewe ni mwanachama wa NLD hivyo ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote kulingana na sifa zake... “Wanalalamika nini hata chama tawala cha CCM, Rais Jakaya Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mkewe Salma pia ni mjumbe wa Nec.”
Alisema Ponela kuwa mkewe hakumfanyi akose haki zake za msingi na kwamba sifa zake na elimu ndivyo vilivyomfanya Rais amteue.
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Florens Turuka alipoulizwa alisema Ikulu haina taarifa za suala hilo lakini wanaamini vyama vya siasa vilikaa na kupendekeza majina manne na kuyawasilisha Ikulu, ndipo Rais alipoteua wajumbe mawili kati yake.

Siku mbili baada ya kuanza kwa Bunge hilo, baadhi ya wajumbe wametaka waongewe posho kwa maelezo kuwa kiasi wanachopewa sasa cha Sh300,000 kwa siku hakiwatoshi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha Dodoma.
Wajumbe hao walitoa kauli hiyo jana katika kikao cha kuwasilisha na kujadili rasimu ya kanuni za Bunge hilo ambacho kilianza saa nne asubuhi.Kwa kiasi kikubwa, kikao hicho ambacho awali waandishi wa habari walizuiwa kuingia, kilitawaliwa na hoja ya kuongezwa kwa posho za wajumbe na kuungwa mkono na wajumbe wengi bila kufuata utaratibu maalumu uliokuwa ukisisitizwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho.
“Wajumbe wengi walikuwa wakisimama na kutaka kuzungumza bila kufuata utaratibu maalumu. Jambo hilo liligeuza ukumbi wa Bunge kuwa kama soko,” kilisema chanzo chetu. Baadhi ya wajumbe waliopata nafasi ya kuzungumzia nyongeza ya posho hizo ni Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi na Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa.
Katika ufafanuzi wake kwa waandishi wa habari, baada ya kikao hicho kuahirishwa kwa muda, Ndassa alisema: “Bunge ndiyo linalotengeneza Katiba ya nchi. Nasikitika kuwa kiwango cha fedha ambacho tunalipwa ni kidogo na hakitoshi kwa sababu kuishi katika Mji wa Dodoma ni gharama kubwa.”
Ndassa alisema kati ya Sh300,000 wanazolipwa wajumbe hao, posho ya kikao ni Sh220, 000 na 80,000 ya kujikimu na kwamba kiasi hicho hakitoshi.
“Mfano ni siku ya Jumamosi na Jumapili. Katika siku hizo mbili wajumbe wote hawalipwi Sh220,000 za posho za kikao na wakati huohuo wanatakiwa kuwalipa madereva wao, kununua mafuta ya gari, chakula na malazi,” alisema.
Aidha, alisema kitendo cha wajumbe kutakiwa kulipwa Sh220, 000 baada ya kusaini katika kitabu cha mahudhurio mara mbili kwa siku ni sawa na udhalilishaji.
“Nilimweleza mheshimiwa mwenyekiti kwamba wajumbe tupo 600 na kulingana na hali halisi wote hatuwezi kuhudhuria kikao kila siku, zipo siku ambazo baadhi yetu wanakuwa na shughuli nyingine na wapo watakaougua, sasa na hao wasilipwe Sh220,000 kweli?” alihoji.
Alisema Serikali inatakiwa kulitazama suala hilo kwa kina kwa maelezo kuwa linaweza kuibua mvutano unaoweza kusababisha wajumbe hao kushindwa kuijadili Rasimu ya Katiba kama inavyotarajiwa na wengi.
“Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikuwa wakilipwa Sh500,00 kwa siku, lakini wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanalipwa Sh220,000 tena mpaka wahudhurie kikao. Hii siyo sawa kabisa,” alisema.
Alisema madereva wa Tume hiyo ya Katiba walikuwa wakilipwa Sh220,000 kwa siku... “Posho yangu ni sawa na aliyokuwa akilipwa dereva wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Sielewi kabisa maana hata viwango vyetu vya posho ni tofauti na wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar, wao wameongezewa posho.”
Alisema jambo hilo litaibua ubaguzi kwa sababu wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanaweza kuwasilisha malalamiko yao kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na kuongezewa posho lakini wajumbe 201 walioteuliwa na Rais hawana mahali pa kulalamika ili kuongezewa posho.
Pamoja na Ndassa kutotaka kuweka wazi, kumekuwa na madai kuwa wajumbe kutoka Zanzibar wameongezewa Sh120,000 na Baraza la Wawakilishi, hivyo kuwafanya kupata Sh420,000 kwa siku.

Hata hivyo, Katibu wa Baraza hilo, Yahya Khamis Hamad alikana madai hayo akisema hakuna fedha za ziada walizolipwa.
Alisema malipo waliyosaini wakiwa Dodoma yaliyotokana na kuhudhuria vikao vya Kamati za Baraza, lakini si nyongeza ya posho.
Akizungumzia suala hilo Nchambi alisema: “Sisi tumeshazoea maisha ya Dodoma na tunaishi hivyohivyo tu licha ya kuwa fedha ni ndogo. Ila hawa wenzetu ambao ni wageni hali zao ni mbaya.
“Wajumbe wapo hapa kwa ajili ya kutengeneza moyo wa nchi yao na wakati tunakuja hapa Dodoma tulielezwa wazi kuwa tusiende kuishi katika nyumba za wageni za vichochoroni. Sasa kwa mantiki hiyo hiki kiwango cha fedha tunacholipwa kitatosha kweli?
“Hapa bungeni wapo maprofesa walioacha kazi zao zinazowaingizia fedha nyingi na kuja kuandika Katiba. Kitendo cha kuwalipa fedha kidogo kinaweza kuwakatisha tamaa.”
Kificho alihitimisha mjadala huo kwa kusema suala hilo la posho litawasilishwa serikalini kuona namna ya kulifanyia kazi.
Baada ya wabunge kutoka kwenye mjadala huo, Mjumbe, Kabwe Zitto alisema anasikitika kwamba tangu siku ya kwanza, suala la posho linashika kasi... “Kiukweli inavunja moyo sana… Ni dhahiri wajumbe lazima walipwe lakini malipo ya posho ndiyo kipaumbele kweli?”
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop