Welcome to our online store Portal

Template Information

New Products
Showing posts with label Kampuni mpya ya simu. Show all posts
Showing posts with label Kampuni mpya ya simu. Show all posts

Thursday, March 20, 2014

KAMPUNI MPYA YA SIMU ZA MKONONI YAANZISHWA TANZANIA

unnamed (2)
 Afisa Mtendaji MKuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,jijini Dar,kulia kwake ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham.
unnamed (3)
Pazia likishushwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kampuni hiyo ya simu za mikononi-Smart.”lets talk. 
unnamed (4)
Afisa Mtendaji MKuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar.
unnamed (1)
Pichani kati ni Balozi wa Kampuni hiyo ya simu iliyozinduliwa  jijini Dar,Msanii wa maigizo ya vichekesho atambulikae kwa jina la Hemed Maliyaga a.k.a Mkwere Orijini akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani (shoto) na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham wakiwa katika picha ya pamoja.
unnamed
Viongozi wakuu wa kampuni ya Smart Telecom, Afrika Masharikii wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi waliojipatia zawadi kupitia mtandao huo,baada ya kushiriki kwenye kampeni ya GIVE US A NAME iliofanyika hivi karibuni.
IPS kukuza ujasiliamali wa jamii katika mawasiliano ya simu Burundi, Uganda na Tanzania
Shirika la kuhamasisha viwanda (IPS), chombo na silaha ya maendeleo ya viwanda chini ya mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Aga Khan (AKFED),jana wametangaza kuingia katika soko la mawasiliano la Afrika Mashariki chini ya kampuni iitwayo SMART.
Jina la kampuni ni matokeo ya kura zilizopigwa Afrika Mashariki katika kampeni ya Uvumbuzi. Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo kutaisaidia AKFED kukuza huduma zake za kibiashara kwa jamii katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda, lengo kuu likiwa kuwekeza na kuwahudumia wateja

Mtandao wa IPS una uwanda/uelewa mpana katika sekta ya mawasiliano. Ni washirika wakubwa wa Roshan shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan na pia washirika muhimu katika shirika la Tcell linaloongoza katika kutoa huduma Tajikistan.
IPS pia ni wawekezaji wakubwa na wa pekee waliowekeza SEACOM submarine cable venture in East Africa. Wakati umefika ambao ushirika wa IPS ndani ya SMART utaleta ushirikiano na kuweka record ya ushirikiano wa makampuni ya simu Nepal na Cambodia  na kuwafanya wawe waongozaji katika soko hili.
Kuzinduliwa kwa SMART kutashirikisha uzoefu wa AKDEF katika kuwekeza kwa lengo la kuhamasisha ujasiliamali na ujenzi wa uchumi wa sauti ambao utatoa fursa nyingi za ajira na kuboresha maisha ya watu. Afrika Mashariki. AKFED imewekeza Serena Hotels, Diamond Trust Bank, Jubilee Insurance Group, National Media Group na katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na miundombinu kama vituo vya nguvu ya umeme vya Bujagali na Tsavo.

“Kazi zetu katika mawasiliano kwa njia ya simu hasa Roshan-Asia ya kati ni kuboresha uwekezaji wa jamii katika miundombinu ya jamii, huduma za afya na elimu. Pia kutengeneza biashara yenye mafanikio katika soko ili tuweze kujitofautisha na washindani wengine, Tunatazamia kuwa uwekezaji katika kampuni dada ya AKDN utakua umeenea katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda kwa zaidi ya miaka 100” alisema Lutaf Kassam Meneja wa IPS
SMART itaingia katika masoko haya ikiwa na dhamira ya embrance tamaduni za ndani ili kuboresha jamii wanakofanyia kazi.mfano mzuri wa dhamiri hii ni njia ambayo jina la kampuni lilivyochaguliwa. Kampeni ya Tupe Jina ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka 2013 ikiwahamasisha watu wa Afrika Mashariki kupendekeza na kulipigia kura jina la kampuni.
 Kampeni hiyo iliwavutia zaidi ya watu 70,000 na majina tofautitofauti yalipendekezwa na kupigiwa kura. Mwisho kampeni ililipata jina la SMART ikikusudia kuangalia uvumbuzi wa mawazo katika soko la Afrika Mashariki.
View detail

Saturday, December 7, 2013

KAMPUNI MPYA YA SIM YAINGIA NCHINI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Sekta ya mawasiliano ya simu Tanzania na Afrika Mashariki leo imepata matumaini mapya kufuatia kuingia kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya ubunifu, kwa jamii, na yenye ushindani kuliko zote, kuzinduliwa bila jina.  
Pamoja na ahadi yake ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao wa simu, kampuni hiyo mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya kiubunifu inayotambulika kwa jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu kwa lengo la kuipa fursa Afrika Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa kupiga kura.  

Hii ni kampuni ya kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na haigopi kuamini watu, na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu kufanya hivyo. Hakuna kampuni yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya kusisimua ya siku 10 kabla ya jina kuwekwa hadharani.
“Tupe Jina” ni kampeni itakayoanza Novemba 25, 2013 hadi 4 Desemba 2013  kwa awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa simu na mtandao wa kijamii wa facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika Mashariki inapaswa kuteua majina ambayo wanapenda hii kampuni mpya iitwe.
Mshirki anaweza kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina  kwa njia ya magogo kwenye mtandao wa www.giveusaname.net au kutuma ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina analopendekeza kwenda namba  15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname. Katika awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini majina yote na itatoa majina matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya kipekee na yenye ubunifu.

 Baada ya hapo Afrika Mashariki watapiga kura kwa ajili ya kupata jina bora moja ambalo hatimaye litakuwa jina la kwanza la kampuni hii ya mawasiliano ya simu ambayo daima itakuwa ya kwanza ya Kiafrika Mashariki. Mshindi katika kampeni hii, mtu ambaye atakuwa amechagua jina ambalo hatimaye litakuwa la kampuni atajishindia muda wa bure wa kupiga simu za ndani na SMS bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Zawadi zingine zitakuwa simu za kisasa za ‘smartphone’ na kompyuta za kiganjani (tablets) kwa washiriki wa kampeni hii ya “Tupe Jina”. Kwa muitikio wa Afrika mpya, balozi wa jina hilo ambaye ni mchekeshaji Bw  Hemedi Khalida “Mkwere” atasherehekewa, ambaye amesimama katika mstari wake kwa kipindi cha television cha “Mizengwe” ambacho kinapata kasi kila siku.

Kutokana na wataalam kutabiri kuongezeka kwa pato la taifa la Tanzania kutoka asilimia 4 hivi sasa hadi asilimia 7 mwaka 2015, sekta ya mawasiliano ina nafasi kubwa ya katika ukuaji wa uchumi katika miaka ijayo na kampuni hii mpya ya mawasiliano ya inawakilisha sura ya kasi hii kubwa ya ukuaji.
Tanzania inabaki kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango cha kuingiza simu chini ya asilimia 50 kufikia Juni 2013, jumla ya matumizi ya mawasiliano ya simu nchini humo ni chini ya wastani kwa nchi za Afrika.
Hii kampuni mpya ya simu kwa umuhimu mkubwa itawekeza kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wateja wake kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu kwa watu wa Uganda katika sekta ya afya na hasa katika tiba za kimtandao na vituo vya elimu ya masafa.

Hii tafsiri yake ni kwamba kuwekeza idadi kubwa ya faida katika kuwezesha Afrika Mpya kuzingatia ongezeko la watumiaji wa mawasiliano ya simu, na zawadi bora ambayo kampuni hii inatarajia katika miaka ijayo ni kukuza sekta ya afya.
Kampeni ya “Tupe Jina” itaisha Desemba 4 baada hapo wananchi wa Tanzania watapata nafasi ya kupeleka namba zao wanazopendekeza kabla ya kutangazwa na kuwekwa hadharani kwa jina la kampuni.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop