Welcome to our online store Portal

Template Information

New Products
Showing posts with label MZEE MANDELA. Show all posts
Showing posts with label MZEE MANDELA. Show all posts

Tuesday, December 17, 2013

SANAMU YA MANDELA YAONGOZA KWA UKUBWA DUNIANI


http://azizicompdoc.blogspot.com/Sanamu inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na maridhiano.
Sanamu kubwa zaidi duniani ya Nelson Mandela imezinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria siku moja baada ya rais huyo wa zamani kuzikwa.
Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu wa mita tisa na ina uzani wa tani nne unusu. Ilizinduliwa katika bustani la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na maridhiano.
Sanamu hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake.
Bwana Mandela lipewa mazishi ya kitaifa nyumbani alikozaliwa katika kijiji cha Qunu Jumapili
Familia ya Madiba , viongozi wa ANC , viongozi wa Afrika na maafisa wengine wakuu walihudhuria mazishi hayo katika kijiji cha Qunu mkoani Cape Mashariki.
Kifo cha Mandela kilifuatwa na maombolezi ya siku kumi na sherehe za kukumbuka maisha ya Mandela aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.

Bendera ya nchi hiyo ilirejeshwa kupepea katika urefu wake wa kaiwada.
Mandela anakumbukwa kwa juhudi zake za kupatanisha wananchi na kupigia debe msamaha miongoni mwa watu na ndio maana leo ikawa siku iliyotengwa kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu hiyo.
Wakati wa utawala wa wazungu, terehe 16 Disemba ilijulikana kama siku ya kuwakumbuka mashujaa wa Afrikaners walioshinda vita dhidi ya jeshi la Zulu mwaka 1883.
Zaidi ya karne moja baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we Sizwe kupigana dhidi ya utawala wa wazungu.
View detail

Sunday, December 15, 2013

ALICHOKIZUNGUMZA KIKWETE KTK MAZISHI YA MZEE MANDELA HIKI HAPA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa marais waliopewa heshima ya kuhutubia ktk maziko ya Mzee Mandela na kumuelezea vizuri mpigania uhuru huyo wa Afrika ya kusini, kuona hotuba yake fuata kiunganishi hapo chini




View detail

ONA LIVE MAZISHI YA MZEE MANDELA AFRIKA YA KUSINI

Fuatilia mazishi ya Mzee Mandela moja kwa moja kupitia Blog yetu, tumeamua kuwahudumia wadau wa Blog yetu kadri tunavyoweza kwa shukrani zetu kwenu kwa kuendelea kutupa kipaumbele ktk blog za kupata habari za uhakika Bofya hapa kuona Live View detail

Wednesday, December 11, 2013

Wake wa Mandela Winnie na Graca, Naomi Campbell, Bono, Jacob Zuma watoa heshima za mwisho kwa Nelson Mandela

article-2521757-1A052BE200000578-192_964x573
Gari maalum lililobeba mwili wa Marehemu Mzee Nelson Mandela likitokea Hospitalini na msafara kuelekea sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya watu maarufu kutoa heshima za mwisho.
article-2521757-1A052DEA00000578-255_964x966
article-2521757-1A053F1500000578-245_964x504
Raia wa Afrika Kusini wakiwa wamejipanga kando kando ya barabara kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Nelson Mandela.
article-2521757-1A0566FA00000578-998_964x353
article-2521757-1A0541DA00000578-598_964x461
article-2521757-1A056ECD00000578-975_964x619
Mwili wa Mzee Nelson Mandela ukiwasili kwenye jengo lililopo mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria, ambapo utalala kwa siku tatu kuruhusu Raia wote wa Afrika Kusini na Dunia kwa ujumla kutoa heshima zao za mwisho.
article-2521757-1A056EB600000578-301_964x691
article-2521757-1A05436B00000578-868_964x568
article-2521757-1A06339300000578-927_964x622
Mwanamindo wa Kimataifa Naomi Campbell alishindwa kuzuia hisia zake baada ya kuona jeneza la Mzee Nelson Mandela likiwasili kwenye viwanja hivyo tayari kwa kutoa heshima za mwisho.
article-2521757-1A064CA200000578-759_964x536
Naomi Campbell akionekana kuto amini kwa kile alichokiona.
article-2521757-1A062AA200000578-705_964x812
Mzee Nelson Mandela enzi za uhai wake alikuwa akimpenda Mwanadada huyu na kumuona kama mjukuuu wake.
article-2521757-1A06419200000578-890_964x492
Bono akitoka kutoa heshima zake za mwisho kwa mzee Nelson Mandela huku akiwa maembatana na Mkewe Ali Hewson (left) pmoja na aliyekuwa msaidizi wa Mzee Mandela Zelda le Grange.
article-2521757-1A0639BA00000578-991_964x721
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiwa ameongozana na wajane wa Mzee Nelson Mandela kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye sehemu maalum iliyoandaliwa.
article-2521757-1A06092C00000578-176_964x833
Mke wa kwanza wa Mzee Nelson Mandela akionekana na majonzi mazito akielekea kutoa heshima za mwisho kwa mumewe wa zamani.
article-2521757-1A06380200000578-720_964x646
Rais Jacob Zuma na mkewe wakitoa heshima za mwisho.
article-2521757-1A0683E800000578-793_964x547
Gaazeti la Daily Mail kwenye picha hii ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wamemuita “Dikteta” kutokana na uchu wake wa madaraka hadi leo.
article-2521757-1A0533E900000578-113_964x567
Raia wa Afrika Kusini wakiwa wamejipanga kando kando ya Barabara kwa ajili ya kutoa heshima zao huku wakiimba na kusifu juhudi za Mzee Nelson Mandela kupigania Uhuru wa nchi yao.

View detail

Friday, December 6, 2013

JK ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO KUTOKANA NA KIFO CHA MZEE MANDELA


400847-nelson-mandela
Marehemu Nelson Mandela.
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini  na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea  tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.

“Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa  machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu”. Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea  Mzee Mandela kuwa ni  kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha  kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa  taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
“Mandela  ni mfano bora kwa wanadamu wa  jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake” .Rais ameongeza kusema, “Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela  mahali pema peponi”.
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop