Welcome to our online store Portal

Template Information

New Products
Showing posts with label Sakata la gesi. Show all posts
Showing posts with label Sakata la gesi. Show all posts

Friday, June 6, 2014

NANI ATAFAIDIKA NA GESI YA MTWARA? MAJIBU HAYA HAPA


mabomba ya gesi
Mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Wananchi wanne kati ya watano wanaamini kuwa mafuta na gesi yatawanufaisha wao, watoto wao na nchi yao kwa ujumla. Wakati huo huo, wananchi wanne kati ya kumi (37%) wanaamini kuwa viongozi wa Serikali na matajiri ndio wataofaidika zaidi. Pia, zaidi ya nusu (55%)  wangependa baadhi ya mapato ya mafuta na gesi wapewe wananchi moja kwa moja kama fedha taslimu.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wa utafiti wenye jina la Kusimamia Maliasili: Wananchi wanasemaje? Utafiti huu ulifanywa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu ya mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa.
Utafiti unaonesha kwamba matakwa ya wananchi ni kuwa, angalau kiasi cha mapato ya mafuta na gesi kipelekwe moja kwa moja kwa wananchi. Mwananchi mmoja kati ya watano (20%) angependelea kiasi kikubwa cha fedha kipelekwa moja kwa moja kwa wananchi; wakati wananchi asilimia 18 wangependelea kuwe na mgawo sawa wa mapato kati ya serikali na wananchi. Asilimia 17 wangependelea Serikali ipate asilimia kubwa zaidi ya mapato kwa ajili ya kuendeleza miundombinu na huduma za kijamii na wananchi wapewe kiasi kinachobaki.

Hata hivyo, Watanzania walio wengi (43%)  wangependa mapato yote yaende Serikalini kwa ajili ya kugharamia huduma muhimu. Isitoshe, wananchi walipoulizwa namna wanavyoamini mapato ya rasilimali yanaweza kuleta manufaa kwa Watanzania, nusu yao (46%) walisema mapato yatumike katika kutoa huduma za afya na elimu, na wananchi wanne kati ya kumi (20%) walipendekeza yatumike kwenye miundombinu au kwenye mipango ya kupambana na umaskini (17%).
Linapokuja suala la usimamizi wa maliasili, jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa Tanzania haiangukii kwenye uhanga wa laana ya utajiri wa maliasili. Uzoefu kutoka nchi nyingine unaonyesha kuwepo kwa uwazi kuhusu mapato na mchakato kama kitu muhimu sana katika kuepuka laana hii, pamoja na ushiriki wa wananchi katika kufanya maamuzi yanayohusu namna mapato yanavyosimamiwa.

Hivi sasa, ingawa Watanzania wengi (64%) wanafahamu ugunduzi wa mafuta na gesi, Utafiti wa Sauti za Wananchi ulibaini kuwa Watanzania wawili kati ya watatu (65%)  wangependa kupata taarifa zaidi. Pindi taarifa zinapokosekana, tetesi na uvumi mara nyingi huziba pengo hilo. Ingawa makadirio ya sasa yanasema kuwa uchimbaji mkubwa wa mafuta na gesi hautaleta faida katika kipindi cha miaka saba hadi kumi ijayo, mwananchi mmoja kati ya watatu (36%) anaamini kuwa makampuni ya mafuta na gesi tayari yameshaanza kupata fedha kutokana na ugunduzi huu. Isitoshe wananchi watatu kati ya kumi (28%) hawana uhakika kama tayari kuna mapato kutoka kwenye mafuta na gesi au la. Aina hii ya mapengo kati ya mitazamo na uhalisia, kama haitaangaliwa vizuri, inaweza kusababisha wananchi kutoridhishwa na usimamizi wa maliasili.

Mjadala mwingine mkali umekuwa juu ya nafasi ya makampuni ya ndani na ya nje ya nchi katika kuchimba mafuta na gesi. Wafabiashara wengi wamedai kwa msisitizo upendeleo utolewe kwa makampuni ya Tanzania. Nusu ya Watanzania (52%) wangependa kunufaika na utaalamu wa makampuni ya kigeni katika sekta hii, lakini kwa kushirikiana na makampuni ya ndani ambayo yanapaswa kumiliki hisa kubwa zaidi katika ushirikiano wa kibiashara hio. Mwananchi mmoja kati ya watatu (35%) anaamini kuwa makampuni ya ndani yapewe kipaumbele kwenye zabuni za makubaliano. Aidha, Watanzania sita kati ya kumi (61%) wako tayari kuona mafuta na gesi yakiuzwa kimataifa kwenye nchi zote. Hata hivyo, wananchi watatu kati ya kumi (28%) wanafikiri gesi inapaswa kutumika nchini tu, na mwananchi mmoja tu kati ya ishirini (5%) anafikiri mauzo ya gesi yafanyike nchi za Afrika Mashariki pekee.

Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema “Kama tunataka watu wa Tanzania wanufaike na ugunduzi wa gesi, tunahitaji uongozi wa serikali ulio imara, wenye uwazi na ubunifu. Kuwepo kwa mfuko huru wa utajiri wa taifa ni sehemu moja muhimu ya ufumbuzi. Hata hivyo, tunahitaji kufikiria juu ya njia mbadala, kama vile kupeleka fedha moja kwa moja kwa watu. Jambo la msingi zaidi ni kuweka wazi taarifa, kusikiliza maoni ya wananchi na kuwasiliana ili kujenga imani ya wananchi kufahamu namna fedha za gesi inavyotumika.”
View detail

Wednesday, January 15, 2014

SAKATA LA GESI LAZUA TAHARUKI KTK FIDIA UKONGA

Kamati
Mwenyekiti wa Kamati ya kufatilia malalamiko ya wananchi wa mji mpya relini Bw. Omari Msusa kushoto akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu fidia wanayotakiwa kulipwa huku Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar es Salaam, Bi. Eugen Mwaiposa akimsikiliza kwa makini (Picha na Mpiga Picha Wetu).
mbunge
Mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es salaam, Bi. Eugen Mwaiposa (kulia) akisikiliza malalamiko ya wananchi wea eneo la Mji Mpya Relini jimboni kwake jana wakilalamika kutaka kulipwa fidia ndogo ambazo hazilingani na thamani ya nyumba zao (Picha na Mpiga Picha Wetu).
mwenyekiti mtaa
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mjipya Relini,Ilala Dar es Salaam Bw. Geofrey Chacha (aliyesimama) akitoa malalamiko ya wananchi mbele ya mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa wa pili kushoto wanaolalamikia kuhusu tahmini ya fidia ndogo inayopitishwa ili kupisha upanuzi wa bomba la gesi linalotoka Mtwara. (Picha na Mpiga Picha Wetu)

Wananchi wa Mji mpya Relini wilaya ya Ilala waliopitiwa na mradi ya bomba la gesi ya Mtwara wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa awasilishe bungeni hoja ya kukataa mradi huo kutokana na kupunjwa fidia ya nyumba na mali zao wanayotakiwa kulipwa.
Wakizungumza na kutoa maazimio hayo katika mkutano wa dharura walioitisha na kuhudhuriwa na mbunge wao, wananchi hao walisema awali walikubali mradi huo kwa manufaa ya taifa lakini baada ya kuletewa dodoso la kutathmini mali na nyumba zao wamegundua kuna ujanja unatumika kuwanyima haki na kuwafanya kuwa masikini maisha yao yote.

Waliendelea kudai kuwa mpaka sasa hawajui serikali imemkabidhi nani jukumu la kuthamini nyumba zao kwani kampuni nyingi za ujanja ujanja zimejitokeza kutaka kuwathamini lakini kwa kiwango cha chini ambacho hakiwezi kumpatia makazi mengine.
Bw. Josephat Haule alisema waathirika wenzao katika Kata za Kivule, Pugu Kwalala na Mbande wao wamethaminiwa vizuri na wanatarajia kupata fedha za kujenga nyumba nyingine kutokana na gharama kuwa juu lakini wao nyumba iliyojengwa kwa sh. mil 57 anathaminiwa alipwe sh. mil. 11 na nyumba zenye thamani ya sh. mil. 10 wanataka alipwe sh, mil 3.
Bw. Robert Pius alisema kutoka taarifa ya Serikali itolewe ya kutangaza kupitisha bomba la gesi eneo hilo waathirika wote walisimamisha uendelezaji wa makazi hayo na kusubiri kupewa haki zao lakini ni mwaka wa pili sasa hakuna taarifa zenye ukweli zinazowafikia hivyo kuwafanya waishi kama wanya aina ya digidigi porini,

Mbunge Mwaiposa akizungumza na wananchi hao aliahidi kushirikiana nao kujua ukweli wa kampuni gani iliyopewa jukumu la kuthamini nyumba na mali zao kwani anachofahamu ni kuwa Kampuni ya Kilwa Energy iliyopewa jukumu hilo awali hakiwa na uwezo wa kifedha kuwalipa wananchi kwa wakati.
Aliahidi kushirikiana na Kamati ya wananchi hao kushughulikia madai yao kwenda Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenda kumuona Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwenda kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ikishindikana wanakwenda kumlalamikia Rais Jakaya Kikwete.
Alisema wananchi wanateseka kwa vile kuhamisha makazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kunarudisha maendeleo nyuma na kama anavyofahamu Serikali ya Rais Kikwete ni sikivu na yenye kufanya kazi kwa ufasaha hajui sababu za wananchi wake kushindwa kutimiziwa ahadi zao katika kiwango kinachostahili.

“Wananchi wangu wanadhiki, wanashida ya fedha lakini si kwa malipo kidogo kiasi hicho, tunapiga picha tuoneshe umma thamani ya nyumba na kiasi wanachotakiwa kulipwa ili wakaendelee na maisha yao sehemu nyingine” alisema Bi. Mwaiposa.
Bi. Mwaiposa alikiri kuona nyumba zilizothaminiwa kwa fedha kidogo ambazo haziwezi kununua kiwanja kingine ambavyo kwa sasa katika maeneo hayo vinauzwa kati ya sh. mil. 10 mpaka sh. mil. 15 kwa kiwanja cha nusu hekari.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop