Monday, December 10, 2012

HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM

 
Ndugu wananchi wa Mkoa wa
Dar es Salaam,
 
Tarehe 11/12/2012 siku ya Jumanne kutakuwa na Sherehe za makabidhiano ya majengo ya huduma za mama na mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Sinza na Rangi tatu.Makabidhiano hayo yatafanywa na Balozi wa Korea kusini kwa niaba ya watu wa Korea Kusini kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Ndugu wananchi wa Mkoa wa
Dar es Salaam,
Makabidhiano hayo yataanzia katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo katika Wilaya ya Ilala kuanzia saa 2:30 asubuhi mpaka saa 5:00 asubuhi.Baada ya hapo makabidhiano hayo yataelekea katika hospitali ya Sinza iliyopo katika Wilaya ya Kinondoni kuanzia saa 5:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana na kuishia katika hospitali ya Rangi Tatu iliyopo katika Wilaya ya Temeke kuanzia saa 7:00 mchana mpaka saa 9:00 alasili.
 
Ndugu wananchi wa Mkoa
wa Dar es Salaam,
Wakati huo huo,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete atazindua na kukabidhi nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto zilizojengwa katika eneo la Msongola lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Makabidhiano hayo yatafanyika kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni.
Ndugu wananchi wa Mkoa
wa Dar es Salaam,
Nawaomba mfike kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya majengo ya huduma za mama na mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Sinza na Rangi tatu pamoja na uzinduzi na kukabidhi nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Said Meck Sadiki
MKUU WA MKOA WA
DAR ES SALAAM
10/12/2012
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About