Tuesday, December 11, 2012

Hali ya taharuki yatanda Misri

Jeshi limeshika doria kila pemba na kuzuia watu kuingia ikulu ya rais
Hali ya usalama iimeimarishwa kote nchini Misri huku Cairo ikijiandaa kwa maandamano mengine yanayowahusisha wafuasi na wapinzani wa katiba mpya iliyopitishwa na serikali ya Misri.
Wanajeshi wanashika doria kwa kutumia vifaru huku wakiwa wameweka vizuizi vya seng'enge na matofali, nje ya ikulu ya rais Mohammed Morsi.
Makundi ya upinzani yanataka afutulie mbali kura ya maoni iliyopangwa kufayika siku ya Jumamosi juu ya katiba hiyo mpya.
Wafuasi wa bwana Morsi wameitisha maandamano yao kufanyika sambamba na yale ya upinzani.
Rais Morsi anasema kuwa katiba mpya italinda faida zilizotokana na mapinduzi ya kiiraia yaliyomwondoa mamlakani rais Hosni Mubarak mwaka jana, lakini wapinzani wake wanasema anarejesha nchi nyuma, katika mizizi ya kidikteta.
Siku ya Jumatatu, kulikuwa na taarifa za ghasia na vurugu mjini Cairo, huku wapinzani waliokuwa wamekesha katika medani ya Tahrir wakifyatuliwa risasi.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About