Tuesday, December 11, 2012

Mamilioni ya noti mpya zapotea Nigeria

  Noti mpya za Nigeria
Kampuni inayochapisha noti kwa ajili ya benki kuu ya Nigeria inajaribu kubaini ni vipi noti mpya zenye thamani ya dola zaidi ya milioni kumi na tatu zilipotea.
Kampuni ya Nigeria ya usalama na uchapishaji wa pesa imemfuta kazi kwa muda mkurugenzi wake na mkuu wa usalama huku ikiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Shirika la kupambana na ufisadi Transparency International, liliiweka Nigeria nambari Thelathini na tano miongoni mwa nchi zenye ufisadi zaidi duniani lakini serikali inapinga hilo.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About