Friday, December 21, 2012

Mahakama ya ICTR yatoa hukumu ya mwisho

Mabakai ya watu waliouawa nchini Rwanda
Mabakai ya watu waliouawa nchini Rwanda

Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Rwanda, imemhukumu mmoja wa washukiwa wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda kifungo cha miaka 35 gerezani.
Hukumu hiyo imetolewa dhidi ya Augustin Ngirabatware, ambaye alikuwa waziri katika serikali ya zamani ya Rwanda.
Ngirabatware ndiye mtu wa mwisho kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kimataifa kuhusu mauaji ya Rwanda ICTR, ambayo kuanzia hi leo itaanza kusikiliza kesi za rufaa.
Takriban watu laki nane wengi wao wa Kabila la Watutsi na Wahutu waliuawa kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda yaliyodumu kwa siku mia moja nchini Rwanda.
Mahakama hiyo ya ICTR ilimpata na hatia Ngirabatware, ya kuhusika na mauaji, kuchochea wapiganaji wake kutekeleza mauaji ya halaiki,ubakaji na ukatili dhidi ya binadam.
Jaji William Hussein alisema'' Mahakama hii imekuhukumu kifungo cha miaka 35 gerezani kutokana na uhalifu uliotenda''
Ngirabatware, alikuwa waziri wa mipango katika serikali ya kihutu ilitokuwa madarakani wakati mauaji hayo yalipotokea.
Ngirabatwarealikamatwa nchini Ujerumani mwaka wa 2007 na kusafirishwa zaidi ya mwaka ammoja baadaye hadi mahakama ICTR mjini Arusha Tanzania.
Mahakama hiyo ya ICTR imewahukumu washukiwa 55 na kuwaachilia huru washukiwa wanane tangu ilipoundwa chini ya azimio la Umoja wa Mataifa Novemba mwaka wa tisini na nne.
Mahakama hiyo itasitisha shughuli zake mwaka wa 2014 baada ya kusikiliza kesi za rufaa 16 zilizowasilishwa mbele yake.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About