Welcome to our online store Portal

Template Information

Thursday, December 20, 2012

Habre kufunguliwa mashtaka-Senegal

Hissene Habre

Hissene Habre aliyekuwa rais wa Chad

Wabunge wa Senegal, wameidhinisha sheria ambayo itaruhusu kuundwa kwa mahakama maalum ya Muungano wa Afrika kumfungulia mashtaka aliyekuwa kiongozi wa Chad Hissene Habre.
Habre mwenye umri wa miaka sabini amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani tangu mwaka wa 2005, nchini Senegal, ambako alitorokea baada ya kuondolewa madarakani mwaka wa 1990.
Kiongozi huyo wa zamani amekanusha madai ya kuhusika na mauaji na dhuluma dhidi ya maelfu ya wapinzani wake.
Mwandishi wa BBC nchini Senegal anasema uamuzi huo, ni habari njema kwa mashirika ya kutetea haki za kibinadam ambayo, yamekuwa yakishinikiza serikali ya nchi hiyo kumfungulia mashtaka kiongozi huyo wa zamani wa Chad kwa miaka kadhaa.
Malumbano makali yamekuwa yakiendelea njini Senegal kuhusu hatma ya Bwana Habre, huku serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo Abdoulaye Wade ikibadili msimamo wake mara kadhaa ikiwa itamfungulia mashtaka au la.

Mashirika ya kutetea haki yaafiki uamuzi wa kumshtaki Habre

''Katika kipindi cha miaka minane, serikali ya Rais Macky Sall, imeafikia mambo mengi hasa kuhimiza waathiriwa walioteswa wakati wa utawala wa miongo miwili wa rais Habre kulipwa fidia kutokana na uvumilivu wao'' Alisema Reed Brody afisa mmoja wa shirika la kutetea haki za kibinadam lililo na makao yake nchini Marekani la Human Rights Watch.
Hissene Habre
Hissene Habre aliyekuwa rais wa Chad

Mashtaka hayo yanatarajiwa kuanza mwaka wa themanini na mbili wakati Bwana Habre alipotwaa uongozi wa taifa hilo baada ya kupindua serikali ya nchi hiyo hadi mwaka wa tisini wakati alipoondolewa madarakani.
Bunge la Senegal lilipitisha sheria hiyo kufuatia makubaliano ya mwezi Agosti mwaka huu kati ya Muungano wa Afrika AU na serikali ya nchi hiyo, ya kutenga fedha zitakazotumiwa na mahakama hiyo maalum.
Msemaji wa wizara ya haki nchini Senegal ameiambia BBC kuwa AU sasa itaanza shughuli ya kuwateuwa majaji kuambatana na orodha iliyopendekezwa na waziri wa wizara ya haki.
Rais wa mahakama hiyo anatarajiwa kuteuliwa kutoka taifa lolote la Afrika na inatarajiwa kuwa uchunguzi kuhusu keshi hiyo itadumu kwa muda wa miezi kumi na mitano, ambapo uamuzi utachukuliwa ikiwa Bwana Habre atafunguliwa mashtaka au la.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop