Wednesday, December 12, 2012

Mali yapata Waziri Mkuu mpya

 Waziri mkuu wa zamani wa Mali Cheick Modibo Diarra
Mataifa mbalimbali duniani yameghadhabishwa na jeshi la Mali kwa kumkamata na kumlazimisha waziri Mkuu wa nchi hiyo Cheick Modibo Diarra kujiuzulu.
Marekani imesema kukamtwa kwa bwana Cheick Modibo Diarra ni pigo kwa utawala wa kidemokrasi nchini Mali.
Kadhalika Umoja wa Mataifa umeitishia kuiwekea Mali vikwazo nayo serikali ya Ufaransa iimesema kuwa panahitajika jeshi ambalo litakaloleta uthabiti katika taifa hilo.
Rais wa Mali sasa amemteua Django Sissoko kuwa waziri Mku mpya.
Tofauti na Jeshi, Bwana Diarra alikuwa amependekeza kuhusisha jeshi la Afrika Magharibi ili kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wanaodhibiti sehemu ya kaskazini.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About