Monday, December 24, 2012

Mamlaka ya Puntland yawakomboa mateka


Haramia wa Kisomali 
Wakuu wa jimbo la Somalia lililojitenga, Puntland, wanasema wameweza kuwakomboa mahabusu zaidi ya 20, waliotekwa na maharamia karibu miaka mitatu iliyopita.
Wanasema kuwa askari wanaolinda mwambao wa Puntland pia wameikomboa meli ya MV Iceberg One iliyosajiliwa Panama, na kwamba hawakuhitaji kutumia nguvu.
Ni jambo la nadra kwa askari wa Somalia kujaribu kukomboa meli kutoka kwa maharamia.
Meli hiyo ilitekwa na maharamia nje ya Yemen mwaka wa 2009.
Wakuu wa Puntland wanasema mahabusu walionekana waliteswa. Wengi wao ni wagonjwa, ambapo haishangazi kwa sababu wamekuwa kizuizini tangu mwezi Marchi, 2010.
Kikosi cha wanamaji wa Puntland kimeizingira meli hiyo kwa karibu majuma mawili.
Pia waliwauwa maharamia kadha waliowagundua kwenye mashua wakipeleka silaha na chakula katika meli hiyo iliyotekwa nyara.
Mashambulio ya maharamia nje ya pwani ya Somalia yamepungua katika miaka miwili iliyopita, kwa sababu meli zinazopita huko zimezidisha ulinzi, na ushirikiano baina ya mataifa yanayopiga doria katika eneo hilo.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About